Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko China kuchangia 98 Bil. ujenzi makao makuu ya ulinzi Dodoma
Habari Mchanganyiko

China kuchangia 98 Bil. ujenzi makao makuu ya ulinzi Dodoma

Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania
Spread the love

SERIKALI ya China imepanga kutoa Yuan RMB 300 Milioni (Tsh. 98,084,910,435.8), kwa ajili ya kuimarisha ulinzi nchini ikiwemo, ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa, jijini Dodoma. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Hayo amesema Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Majeshi nchini, leo tarehe 25 Novemba 2019 katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa makao makuu hayo, iliyofanyika Kikombo, Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

Jenerali Mabeyo amesema sehemu ya fedha hizo zitatumika kujenga makao makuu yanayokidhi viwango vya kimataifa, ambapo kutakuwa na  ofisi maalumu ya Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi, kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake ya ulinzi wa taifa.

Mkuu huyo wa Majeshi amesema China imetenga fedha hizo, baada ya Tanzania kuiomba msaada wa kuboresha dhana za jeshi na ujenzi wa makao makuu hayo.

“Ombi la tatu kwa China ilikuwa ni ujenzi wa eneo hili la makao makuu, yanayokidhi viwango vya kimataifa. Kwa maana kwamba, Amiri Jeshi Mkuu anaweza akafanyia kazi hapa, akatekeleza majukumu ya kiulinzi akiwa katika makao makuu ya kiulinzi,” amesema  Jenerali Mabeyo na kuongeza;

“Kwa maana unakuwa na ofisi maalumu hapa, ya kutoa maekelezo ya kiulinzi. Naomba nikufahamishe kwamba, marafiki zetu walikubali na kwa sasa hivi tayari wametenga RMB 300 milioni.”

Wakati huo huo, Jenerali Mabeyo amempongeza Rais John Magufuli kwa kuafiki ujenzi wa makao makuu hayo, pamoja na juhudi zake katika kuimarisha utendaji kazi wa majeshi nchini, pamoja na kuboresha maslahi ya askari wa jeshi.

Jenerali Mabeyo amesema Jeshi linamuunga mkono kwa hatua anazochukua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

Habari Mchanganyiko

Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Greyhorse zasaini mkataba wa bil.7.4

Spread the loveTAASISI ya Mwalimu Nyerere (MNF) imesaini mkataba wa miaka 10...

error: Content is protected !!