June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chile bingwa Copa Amerika, washinda kwa penalti 4-1

Wachezaji wa timu ya Taifa ya Chile wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe

Spread the love

WENYEJI wa fainali za Copa America, Chile wametwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuwafunga Argentina kwa hatua ya mikwaju ya penalti katika mchezo mgumu wa fainali.

Timu hizo mbili zilitoka suluhu katika dakika 90 za kawaida na hata baada ya dakika 30 za nyongeza bado matokeo yalisomeka 0-0.

Hakukuwa na njia nyingine ya kumpata mshindi zaidi ya kupisha hatua matuta ambapo Chile wakaibuka wababe kwa penalti 4 kwa 1.

Lionel Messi alijikuta akikatwa sana kiatu katika muda mwingi wa mchezo kutoka kwa mabeki wa Chile huku Angel Di Maria akitolewa dakika ya 29 baada ya kuumia.

Wafungaji wa penalti za Chile walikuwa ni Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Aranguiz na Alexis Sanchez wakati penalti pekee ya Argentina iliyotinga wavuni ni ile ilipigwa na Lionel Messi wakati waliokosa kwa Argentina ni pamoja na mshambuliaji wake hatari, Gonzalo Higuain nana Ever Banega.

error: Content is protected !!