January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chikawe akwepa lawama mauaji ya albino

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akiwa katika uzinduzi wa kampeni ya Inatosha mauaji ya albino

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe akiwa katika uzinduzi wa kampeni ya Inatosha mauaji ya albino

Spread the love

MATHIAS Chikawe-Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amekwepa lawama. Anawataka wananchi kuacha tabia ya kunyooshea  kidole na kuilalamikia Serikali na vyombo vya dola kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino). Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Anasema “serikali peke yake haiwezi kufanya kazi hiyo bali kwa kushirikiana na wananchi. Waswahili wanasema ukitaka kumfukuza kichaa nyumbani kwako hakikisha unamfukuza na makopo yake yote, kwa hivyo basi tukitaka kuwakomesha hawa wauaji wa Albino ni lazima tushirikiane kuazia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla, kila mmoja awajibike kuwalinda.”

Chikawe amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za kuzuia mauaji ya Albino, “IMETOSHA FOUNDATION”  yaliyofanyika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa serikali imeendelea kulipa uzito swala hilo bila kuchoka na mahakama kwa upande wake imeendelea kutoa ushirikiano, ambapo kwa mwaka 2006 hadi 2015  watuhumiwa  139 wameshakamatwa.

Amewahakikishia Albino kuwa, serikali ipo pamoja nao, na kwamba hatawaacha tatizo hili kuendelea. “Tutatumia mbinu zetu na  maarifa yote tuliyonayo kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa wote na kukomesha tatizo hili.”

Naye mwanzirishi wa kampeni hizo, Henry Mdimu amesema, aliamua kuianzisha kwa lengo la kutoa elimu juu ya mauaji ya Albino, na kuweza kuwaondoa watu katika fikra mbovu juu ya walevu hao.

“Tutatembea katika mikoa yote ndani ya Tanzania haswa mikoa ambayo inaongoza kwa mauaji hayo. Kuna watu wanadhani Albino sio watu wa kawaida yaani inafikia kipindi  wananchi wezetu wanatunyanyapaa, mtu anamtumia Albino kumtishia mtoto wake kula chakula,” ameeleza Mdimu.

error: Content is protected !!