January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chikawe ajigamba kudhibiti uhalifu

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Mathias Chikawe, leo amejitamba kuwa Wizara yake imejitahidi kuhakikisha vitendo vya uhalifu nchini vimedhibitiwa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Aidha, amesema wamefanikisha hilo kwa kipindi cha miaka 10 katika Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inayokaribia kumaliza muda wake.

Amesema, Jeshi laPolisi limefanikiwa kudhibiti matukio makubwa  ya uhalifu, hususani matukio ya kutumia silaha uliokuwa umekithiri maeneo mbalimbali, ikiwemo ya uvunjifu wa maduka na mabenki.

Amebainisha hayo Jijini Dar es Salaam wakati  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Wizara katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya nne kilichoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

Ameendelea kusema  kuwa, mwaka 2006 baada ya serikali ya  CCM kuingia madaraka kulikuwa na matukio manne ya wizi kwa kutumia silaha katika mabenki, ambamo kwa sasa wamedhibiti hilo pamoja na kufunga mtandao wa uhalifu baina ya Tanzania na nchi jirani.

Anajisifu kuwa  mafanikio ambayo wizara imepata pamoja na, kukamata madawa ya kulevya kilo 2,022 na gram 334.5 na watuhumiwa 6,944, mirungi na bangi ni, kilo 871,632 na gramu 990.452 na ekari 792 za mashamba ya bangi.

Amesema  Wizara imefanikiwa kudhibiti kuzagaa kwa silaha ndogondogo za kukabiliana na uhalifu wa kutumia silaha, ambapo wamekamata jumla ya silaha 6,693 na watuhumiwa 5,909, risasi jumla ya 62,487 na watuhumiwa 592 kukamatwa.

Hata hivyo, jumla ya silaha 80,150 zimehakikiwa na kati ya hizo 62,650 kumbukumbu zake zimeingizwa katika jeshi la polisi ambapo jumla ya askari 105 wamepewa mafunzo maalumu ya kutumia silaha.

Amesema  wamefanikiwa  kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani kwa kufanikiwa  kujenga mabweni mapya kutoka 22,669 hadi 29,552.

Amesema kwa upande wa wakimbizi  wizara imewarudisha kwao wakimbizi wapatao 456,371 kutoka sehemu mbalimbali.

Chikawe amesema, katika kipindi hiki wamewakamata wahamiaji haramu 27,893 na kuwachukulia hatua mbalimbali za kisheria, na katika kutekeleza hilo, wahamiaji haramu 30,872 wameondolewa nchini.

“Kuhusu suala la amani na utulivu hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, wananchi wawe na amani kabisa Jeshi la polisi liko macho muda wote ninauhakika wa kuimarisha ulinzi,” amesema

error: Content is protected !!