July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chifu Bilingi aimaliza kabisa Dodoma

Spread the love

DIWANI aliyemaliza muda wake kupitia Chadema kata ya Dodoma Makulu, Chifu Ally Bilingi amewataka wananchi wa kata hiyo kuhakikisha wanamchagua mbunge wa Chadema Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila, Rais Edward Lowassa na Diwani wakata hiyo Pascal Matulaa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo Chifu Bilingi amesema kama wananchi watafanya makosa na kudanganywa ikafika hatua wakaichagua CCM kata hiyo itarudi nyuma kimaendeleo na hakuna mtu ambaye ataweza kumiliki ardhi wala nyumba kama ilivyo sasa.

Alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara wa kampeni za ubunge na udiwani uliofanyikia katika viwanja vya karibu na shule ya msingi ya Makulu.

Chifu Bilingi ambaye ni nguli wa siasa mjini hapa na awali alikuwa kada wa CCM na kuwa diwani kwa miaka 15 akiwa CCM ambapo mwaka 2010 alijiengua CCM na kujiunga na Chadema na kuendelea kuwa diwani kwa kipindi cha miaka 5, amesema kata hiyo inatakiwa kuongozwa na watu wapenda mabadiliko na siyo viongozi wa CCM.

Katika mkutano huo wa kampeni Chifu Bilingi amesema kwa kipindi cha miaka 15 ambayo alikuwa diwani wa CCM hakuweza kuwafanyia wananchi mambo makubwa ya kimaendeleo kutokana na urasimu uliopo ndani ya chama tofauti na miaka 5 ambayo amewatumikia wananchi akiwa Chadema.

Akimnadi mgombea ubunge kwa kupitia Chadema, Chifu Bilingi amesema Kigaila ni kiongozi ambaye anafaha kwa kuwatetea wananchi kwani hata kabla ya kuwa na ndoto za kugombea ubunge Dodoma Mjini amekuwa akiwatetea wananchi kuhusu umiliki wa ardhi yao jambo ambalo lilimsababishia kufunguliwa kesi pamoja na kuwekwa rumande.

“Kigaila ninamfahamu vizuri ametusaidia sana kutetea ardhi yetu ambayo mara kadhaa tunapolwa na serikali kupitia Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu (CDA) lakini nyinyi mnakumbuka sana alivyopambana na kuwekwa ndani na kufunguliwa kesi mbalimbali lakini bila kuwa na wakili tulishinda kesi,” amesema Chifu Bilingi.

Mbali na hilo amesema iwapo atachaguliwa Diwani wa Chadema na rais wa Chadema pamoja na mbunge wa Chadema ni wazi kuwa manyanyaso yanayotokana na uonevu wa umiliku wa ardhi utakuwa umekwisha.

Kwa upande wake mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Benson Kigaila amesema hakuna sababu yoyote ya watanzania hususani wakazi wa kata ya Dodoma Makulu pamoja na maeneo mengine kutomiliki ardhi yao.

Amesema kwa sasa wananchi wa Dodoma wanasumbuliwa na mnyama mkubwa ambaye anaitwa CDA kwani wananchi hawana uhakika wa kumiliki ardhi yao na nyumba zao.

Mbali na hilo amesema ni masikitiko makubwa kuona nyumba za watu zinavunjwa lakini hawapatiwi fidia kwa maelezo kwamba watu hao ni wavamizi jambo ambalo amesema ni la kihuni.

Amesema kipaumbele chake iwapo atashinda nafasi ya ubunge hatahakikisha wananchi wanamiliki ardhi na wale wote ambao walibomolewa nyumba zao bila fidia lazima wapewe fidia ambayo inaendana na wakati wa sasa.

Naye mgombea udiwani kwa kupitia Chadema, Pascal Matulaa amesema kata hiyo ni kati ya kata ambayo inaonesha kuonewa na serikali kutokana na kutokuwepo kwa juhudi za makusudi za upimaji wa viwanja kwa wakati.

Jambo lingine amesema viwanja bado vinauzwa kwa bei ya ghali na kutokana na hali ya sasa hakuna mwananchi ambaye anaweza kumudu ya kununua kiwanja kwa kiwango ambacho kinatajwa licha ya kuwa kiwanja hicho kinaporwa kwa mwenywe kiwanja au shamba na kuuzwa kwake au kuuzwa kwa mtu mwingine.

error: Content is protected !!