December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Cheo cha shahidi chahojiwa mahakamani kesi ya Mbowe

Spread the love

 

ASKARI Mpelelezi wa Polisi nchini Tanzania, H4347 Goodluck, ambaye ni shahidi wa pili wa jamhuri katika kesi ndogo ndani ya kesi ya uhujumu uchumi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, amehojiwa iwapo amepandishwa cheo kutokana na kushiriki tukio la kuwakamata watuhumiwa wawili wa kesi hiyo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelsa).

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala  amemuuliza swali hilo leo Jumanne, tarehe 23 Novemba 2021, katika mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Mawasiliano jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Ni baada ya shahidi huyo kuieleza mahakama hiyo namna alivyoshiriki kuwakamata washtakiwa wawili katika kesi hiyo, Adam Kasekwa na Mohammed Abdillah Ling’wenya, tarehe 5 Agosti 2020, maeneo ya Rau Madukani mkoani Kilimanjaro.

Mahojiano yao yalikuwa hivi;

Kibatala: Nimesikia una cheo tofauti na ulichokuwa nacho wakati unawakamata watuhumiwa wawili?

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Umeshuka au umepanda?

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Nitakuwa sahihi nikisema baada ya matukio haya yamekupandisha cheo?

Shahidi: Sio sahihi, elimu yangu imenipandisha cheo, na  sio baada ya kazi niliyofanya ndiyo nimepanda cheo.

Kibatala: In terms of time cheo kimekuja baada ya kufanya kazi hiyo?

Shahidi: Siyo sahihi,  imekuja kutokana na elimu yangu

Kibatala: Ni sahihi tukio lilianza na kikafuta cheo?

Shahidi: Sio sahihi, sababu nimepa kwa  sababu ya elimu yangu

Jaji Tiganga: swali lake ni baada?

Shahidi: Hapana

Kibalata: Ulipanda cheo tarehe ngapi?

Shahidi: Nilipanda  cheo tarehe 23 Agosti 2021

Kibatala: Na ilikuwa kabla?

Shahidi: Bada ya kukamata watuhumiwa

Kibatala: Baada ya kupanda cheo cha awali na mmeibua nyie wenyewe, Wakili Hilla  alikuongoza kufafanua namna ulivyopanda cheo labda kutokana na elimu yako, alikuongoza kufafanua?

Shahidi: Hapana

Kibatala alimuuliza swali hilo baada ya askari huyo wakati akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Pius  Hilla, alipodai kuwa alipandishwa cheo tarehe 23 Agosti 2021.

Goodluck alidai yeye ni askari polisi tangu 2013 alipoajiriwa na Jeshi la Polisi, na kwamba anafanya kazi katika Kituo Kikuu cha Polisi Arusha, Idara ya Upelezi wa Makosa ya Jinai.

Wakili Hilla alimuongiza shahidi huyo kama ifuatavyo;

Hilla: Sasa hivi una cheo gani

Shahidi: Hivi sasa ni Sergent

Hilla: Ulikioata lini?

Shahidi: Nilikipata tarehe 23 Agosti 2021

Hilla: 2020 ulikuwa na cheo gani?

Shahidi: Polisi Constable/Detective

Hilla: Vipo daraja gani?

Shahidi: Idara ya Upelelezi Makosa ya Jinai

Hilla: Ni muda gani uko kwenye hiyo idara?

Shahidi: Nina muda wa miaka mitatu

Hilla: Majukumu yako ni nini?

Shahidi: Majukumu yangu ni kukamata wahalifu, kufanya upelelezi, kukusanyavielelezo na kitekeleza majukumu mbalimbali ninayopewa na viongozi wangu.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI TV, MwanaHALISI Online na mitandao yetu kujua undani wa kesi hiyo ambayo shahidi anaendelea kutoa ushahidi wake

error: Content is protected !!