January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chenge kuiburuza CCM mahakamani

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge

Spread the love

MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, yuko njiani kukifikisha mahakamani Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaripoti Saed Kubenea… (endelea).

Anapinga kusimamishwa ujumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa (NEC) wa chama hicho.

Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na uenezi, alitangaza mwishoni mwa wiki kuwa Chenge na wenzake wawili – Prof. Anna Tibaijuka na William Ngeleja – wamesimamishwa uongozi ndani ya chama hicho.

Prof. Tibaijuka ambaye ni mbunge wa Muleba Kusini, amesimashwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC). Naye Ngeleja aliyeshikilia ubunge katika jimbo la Sengerema, ni mjumbe wa NEC.

Alisema, viongozi hao watatu wamesimamishwa uongozi kwa makosa ya maadili; hatima ya uongozi wao utajulikana baada ya vikao vya maadili kumaliza kazi zake.

Chenge hakupatikana kufafanua madai hayo kwa kutwa nzima ya jana-simu yake kili ilipopigwa, ilijibiwa kuwa “ahasante kwa kutumia mtandao wa Vodacom, huduma kwa mteja unayempigia zimezuiwa kwa muda-jaribu tena baadaye”.

Mtoa taarifa anasema, Chenge ameamua kwenda mahakamani baada ya kujiridhisha kuvunjwa kwa taratibu katika kufikia maamuzi hayo. Hakuzitaja taratibu hizo.

Amesisitiza, “Ni lazima Chenge atakwenda mahakamani kuomba amri ya kuzuia uamuzi huu wa CCM. Kesi hii, itafunguliwa mara baada ya kukabidhiwa barua inayomjulisha kuhusu uamuzi huo.”

Chenge, Prof. Tibaijuka na Ngeleja, wanatuhumiwa kujipatia “mgawo” wa mabilioni ya shilingi, kutoka kwa James Rugemalira, mmoja wa wanahisa katika kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Rugemalira alikuwa akimiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni hiyo, kupitia kampuni yake ya VIP Engineering and Marketing ya jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!