Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Chembechembe za plastiki hatari kwa afya
Habari Mchanganyiko

Chembechembe za plastiki hatari kwa afya

Spread the love

 

UTAFITI uliofanywa kuhusu chembechembe zitokanazo na plastiki zinazopatikana kwenye fukwe za bahari zimeonesha kuwa na kemikali za sumu ambayo inaweza kusababisha madhara ya kiafya kwa binadamu. Anaripoti Selemani Msuya, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na Utunzaji wa Bioanuai Tanzania (TABIO), Abdallah Mkindi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti huo uliofanyika kuanzia mwaka 2020 kwa kushirikisha nchi 35 duniani.

Mkindi alisema utafiti huo uliofanywa katitika nchi 35 kupitia mashirika ya ndani ya TABIO na AGENDA, na ya Kimatiafa ya International Pollutants, Elimination Network (IPEN), International Pellet Watch (IPW) ambapo matokeo ya utafiti yanaonesha Tanzania haijaadhirika kwa kiwango kikubwa.

“Utafiti uliofanywa umebaini kwenye chembechembe za plastiki ambazo zimekutwa katika fukwe kuna kemikali za sumu aina ya Ultraviolet (UV) stabilizers na Polychlorinated Biphenyls (PCBs) ambapo uchunguzi iligundua aina 11 za Bisphenol A nasita za UV,” ulisema utafiti.

Alitaja mabara yaliyohusika na utafiti huo kuwa ni Afrika, Amerika ya Kusini na Kaskazin, Asia, Australia, Karibian na Ulaya ambapo matokeo yanaonesha kemikali hizo zipo.

“Nchi baadhi ambazo zimehusishwa na utafiti huu I Kenya, Tanzania, Senegal, Morocco na nyingine za mabara mengine,” alisema.

Alisema baada ya kukusnaywa kwa chembechembe hizo kwenye fukwe za Bahari ya Hindi eneo la Dar es Salaam walipeleka katika maabava ya kimataifa iliyoko Jamhuri ya Czech na matokeo yameomesha chembechembe hizo plastiki zina kemikali zenye sumu ambazo zinaweza kuchangia magonjwa kama saratani.

“Utafiti ambao tumefanya kwa kushirikiana na wadau wengine kuhusu hizi plastiki zinazopatikana kwenye fukwe zetu zina kemikali zenye sumu, hivyo juhudi zinahitajika kuhakikisha madhara yake hayawi makubwa kwa siku za mbeleni, pamoja na ukweli kuwa Tanzania hakuna madhara makubwa,” alisema.

Mratibu huyo aliomba taasisi kama Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) na nyingine ambazo zinahusika na uchunguzi wa kemikali kuhakikisha wanachunguza plastiki hizo ili kunusuru jamii ya Kitanzania.

Alisema kiuhalisia elimu kuhusu chembechembe hizo haijatolewa ya kutosha hivyo anaamini mamlaka hizo za Serikali zikijikita kutoa elimu wananchi wataweza kujikinga zaidi na madhara yake.

Mkindi alisema chembechembe za kemikali zenye sumu ambazo zimebainika katika utafiti huo ni pamoja na zile ambazo zimepigwa marufuku kupitia Mkataba wa Stockholm Sweeden kutokana na kuwa na madhara.

Aidha, alisema utafiti huo umeonesha kuwa baadhi ya chembechembe hizo zinatokana na plastiki zilizofanyiwa urejelesho, hivyo mamlaka za usimamizi zikiweka kipaumbele zitaweza kunusu jamii isiathirike.

“Sisi tunaunga mkono juhudi za Serikali kuzuia matumizi ya plastiki, lakini tunaomba nguvu iongezeke zaidi kuhakikisha zinazozalishwa zizingatie Mkataba wa Stockholm,” alisema.

Alisema pamoja na Afrika kutozalisha plastiki kwa kiwango kikubwa, lakini imeaathirika zaidi kuliko mabara mengine jambo ambalo linahitaji ngumu ya pamoja na kupambana na hali hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!