Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari Chemba wapigwa msasa huduma ya afya ya mama na mtoto
Habari

Chemba wapigwa msasa huduma ya afya ya mama na mtoto

Spread the love

 

TAASISI ya Benjamini Mkapa Foundation imeendelea kuyanoa makundi manne ndani ya wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma kwa lengo la kuwapatia elimu kuhusu huduma ya afya ya mama na mtoto. Anaripoti Danson Kaijage – Dodoma… (endelea)

Makundi yaliyopewa elimu kwa lengo la kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto ni waganga wafawidhi wa vituo vya afya, waelimisha rika, watendaji wa vijiji na watoa huduma ya afya ngazi ya jamii (CHW).

Akizungumza katika kufunga mafunzo kwa makundi hayo, Meneja mradi – huduma za afya ya Jamii kutoka katika taasisi hiyo, Happiness Willbroad amesema mafunzo hayo ya siku sita kwa makundi hayo yanalenga kuboresha ufanisi wa utoaji huduma ya afya kwa jamii.

Amesema iwapo makundi hayo yatafanya kazi kwa ushirikiano, huduma ya afya kwa jamii itakuwa imesogea karibu na wananchi na itakuwa bora zaidi.

Pia amesema mafunzo hayo yanalenga kuhakikisha vijana wanapatiwa elimu ya kutosha kwa ajili ya kuwaondoa katika matumizi mabaya ya madawa ya kulevya pamoja na unywaji wa pombe kwa kupitiliza.

Kwa upande wake Afisa Miradi Mwandamizi wa Benjamini Mkapa Foundation, Dk. Daud Olemkopi amesema taasisi hiyo imeanza kutekeleza miradi mbalimbali katika wilaya ya chemba kwa miaka mitatu sasa.

Akizungumzia miradi amesema ni pamoja na utoaji elimu ya huduma ya mama na mtoto, ujasiriamali, madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya, madhara ya mimba za utotoni na madhara ya utumiaji wa pombe za kupita kiasi.

Amesema kwa sasa tayari wanahudumia vijiji 114 katika wilaya nzima ya Chemba kutoa ajira kwa watoa huduma.

Amesema wakati wa kuanza mradi huo ndani ya miaka mitatu akina mama ambao walikuwa wakijifungulia zahanati na vituo vya afya ilikuwa asilimia 47 na sasa kwa miaka mitatu imefikia asilimia 61.

Hata hivyo, amesema bado wilaya ya Chemba bado haijafikia hatua inayotakiwa ya kufikia asilimia 80 ambayo ndiyo viwango vinavyotakiwa.

“Walianza na vijiji 37 sasa wameweza kutekeleza mradi wa vijiji vyote 114 na wamemeingia mwaka wa nne kwa lengo la kuboresha huduma zaidi,” amesema.

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Chemba, Saimon Chacha ameyataka makundi ambayo yamepatiwa mafunzo na Benjamini Mkapa Foundation wanatakiwa kuyafanyia kazi na si vinginevyo.

Aidha, amesema umefika sasa wakati wa kuweka mipango mikakati na mipango kazi kwa nia ya kuhakikisha huduma ya afya inawafikia wananchi kwa wakati na yauhakika.

Amesema wapo baadhi ya watendaji wa vijiji ambao wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa baadhi taasisi mbalimbali za kimaendeleo na wakati mwingine hawana hata mipangokazi ambayo wanaitekeleza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

HabariSiasa

Dk. Rose Rwakatare atoa kadi 500 kila Wilaya Morogoro

Spread the loveMWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk...

ElimuHabari

CBE, WMA wasaini makubaliano wanafunzi kusoma wakifanyakazi

Spread the loveNAIBU Spika Musa Azzan Zungu amekipongeza Chuo cha Elimu ya...

HabariTangulizi

Dk. Slaa, Mwabukusi kuhojiwa na jeshi la Polisi Mbeya

Spread the loveJESHI la Polisi jijini Mbeya, linawashikilia kwa mahojiano Dk. Wilbroad...

HabariHabari Mchanganyiko

Kairuki Hospital Green IVF  yawanoa madaktari kuhusu upandikizaji mimba

Spread the love KITUO cha Upandikizaji Mimba cha Kairuki Hospital Green IVF...

error: Content is protected !!