
Oscar dos Santos
KIUNGO mshambuliaji wa timu ya taifa ya Brazir na klabu ya Chelsea Oscar dos Santos (25), anatarajiakujiunga na klabu ya Shanghai SIPG inayoshiriki ligi kuu nchini China katika dirisha dogo la usajiri mwezi Januari baada klabu zote mbili kukubaliana, anaandika Kelvin Mwaipungu.
Chelsea walitangaza kwenye ukurasa wao kupitia mtandao wa “twitter” kuwa kiungo wao huyo amekubali dili la kwenda nchini china na kumtakia kila la kheri, baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa misimu minne na kuifanikisha Chelsea kutwaa mataji ya kombe la Europa, kombe la ligi na ligi kuu.
Chelsea Football Club and Shanghai SIPG have agreed terms for the permanent transfer of Oscar… https://t.co/7izeugHu1J
— Chelsea FC (@ChelseaFC) December 23, 2016
Baada ya Chelsea kukubali ofa, kocha wa klabu ya hiyo Antonio Conte ameonesha hisia zake juu ya kipaji alicho nacho kiungo huyo na kuondoka kwenye kikosi chake licha ya kutokuwa na nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza lakini bado aliheshimu uwamuzi wake wa kuondoka.
Thank you, @oscar8 and good luck for the future. pic.twitter.com/HYpEPQsWro
— Chelsea FC (@ChelseaFC) December 23, 2016
Oscar ambaye atakwenda kuchukua kitita cha pauni milioni 20 kwa mwaka atakuwa kati ya wachezaji wanaolipwa kiasi kikubwa cha fedha katika ligi hiyo na duniani kwa ujumla, na ataungana na mshambuliaji raia wa Argentina katika ligi hiyo.
Klabu nyingi za nchini china zimekuja kuleta changamoto kubwa katika soka kwa sasa, hasa kwa klabu nyingi barani ulaya na duniani kwa ujumla kwa kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili kuipa thamani ligi yao na kuvutia idadi kubwa ya wawekezaji kutoka kila kona ya Dunia.
More Stories
Yanga yaanza safari ya kutetea ubingwa wake
Ngao ya Jamii kuchezwa kwa mtoano
KMC yatua Arusha kibabe