May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chelsea yapoteza fainali ya kwanza, Leicester bingwa FA

Spread the love

GOLI la Youri Tielemans la dakika ya 63, lilitosha kuipa ubingwa wa kwanza wa FA CUP, timu yake ya Leicester City msimu wa 2021 dhidi ya Chelsea.

Fainali hiyo, imechezwa jana Jumamosi, tarehe 15 Mei 2021, katika Uwanja wa Wembley nchini Uingereza, ikishuhudia Leicester ikibeba kombe hilo lenye heshima kubwa nchini humo.

Chelsea, ambayo mwaka huu, imeingia fainali mbili ya FA na Klabu Bingwa Ulaya (Uefa), imeanza kwa kupoteza ya FA CUP na sasa itasubiri ya Uefa dhidi ya Manchester City.

Leicester City, imetwaa kombe hilo, baada ya kuwa imecheza fainali nne bila mafanikio.

error: Content is protected !!