August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chelsea, Manchester City wapigwa faini

Spread the love

HATIMAYE chama Soka England (FA) imezipiga faini klabu za Manchester City na Chelsea kufuatia wachezaji wao kuhusika kwenye vurugu wakati wa mchezo wa ligi kuu uliokutanisha klabu hizo Disemba 3 kwenye wa Etihad na Chelsea kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Chelsea wao wamepigwa faini ya pauni 100,000 na Manchester City wakipigwa faini ya pauni 35,000 pamoja na mshambuliaji wao Sergio Kun Aguero kupigwa adhabu ya kukosa michezo minne baada ya kumchezea lafu ya makusudi beki wa Chelsea, David Luiz ingawa mwamuzi wa mchezo huo alimuoneshea kadi nyekundu.

Baaada ya maamuzi hayo wachezaji wa timu zote mbili waliingia kwenye taflani kila mtu akitetea maamuzi kwa upande wake kiasi kilichopelekea kiungo wa Manchester City, Fernandinho naye kutolewa nje ya uwanja kwa kadi nyekundu katika dakika saba za nyongeza kwenye mchezo huo baada ya kumakaba koo Cesc Fabregas katika vurugu hizo.

Awali Chelsea walitahadhalishwa na FA kama wangeweza kupokonywa baadhi ya alama kutokana na kuwa na rekodi mbovu ya utovu wa nidhamu kwa wachezaji wao, toka mwaka 2015 klabu hiyo imeshapigwa faini mara sita kwa makosa hayo ya utovu wa nidhamu uwanjani na viongozi wa klabu hiyo kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao.

Chelsea ambayo kwa sasa ni vinara kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kushinda michezo 10 mfululizo na kujikusanyia jumla ya alama 40 tofauti ya alama saba na Manchester City baada ya kutopata matokeo ya ushindi kwa mechi tatu mfululizo na hivyo kukata tama katika mbio za ubingwa kwa msimu huu.

error: Content is protected !!