January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Cheka atambia kambi ya Zambia

Spread the love

BONDIA Francis Cheka amerejea nchini kutoka Zambia alipoweka kambi na kutamba amemaliza kazi ya kuchakaza mpinzani wake, Geard Ajetovic raia wa Serbia katika pambano la Mabara uzito wa super middle la Shirikisho la Masumbwi ya Kulipwa Duniani (WBF). Anaandika Erasto Masalu … (endelea).

Cheka na Ajetovic watapambana kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27, 2016 katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini leo, Cheka amesema mazoezi aliyofanya katika kambi hiyo, ndiyo kiama cha mpinzani wake ambaye hawezi kutoka katika mpambano huyo.

Cheka alimpongeza meneja wake, Juma Ndambile kwa kumwezesha kuweka kambi nje ya nchi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo kwa upande wake.

Amesema kuwa Ndambile ameonyesha kuwa wanajali na wana malengo makubwa ya kumwendeleza kutokana na ukweli kuwa amekaa katika kambi ya kisasa yenye mabondia na makocha wazuri nchini Zambia.

“Kwanza naishukuru kampuni ya Advanced Security Limited kwa kufanikisha kambi hii, nimejifua vya kutosha nchini Zambia, mazoezi yalikuwa magumu na yalihitaji uvulivu mkubwa, kwa kutambua lengo langu ni nini, nilifanya kwa juhudu zote na sasa nipo tayari kwa pambano, hata kesho (leo) nipo tayari kwa bondia yoyote duniani,” amesema Cheka.

Amesema kuwa kutokana na siku kuwa nyingi, ataendelea na mazoezi hapa hapa nchini huku akisubiri mipango mengine ya meneja wake kwa upande wa maandalizi.

Meneja wa Cheka, Ndambile amesema kuwa lengo la kampuni yao ni kufanya mapinduzi na kuleta maendeleo katika mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini.

Ndambile amesema kuwa Cheka ni bondia mwenye kipaji na hakuwa tayari kuona kipaji hicho kinapotea na kuchukua jukumu la kumwendeleza. “Mimi na kampuni yangu tuna mipango ya kuwamiliki mabondia wengi hapa nchini, kama ilivyo kwa Cheka, nao watapata fursa ya kufanya mazoezi nje ya nchi na kupata mapambano ya kimataifa ya ubingwa ili kuiletea sifa taifa,” amesema Ndambile.

Amesema kuwa wanataka kutumia vizuri fursa waliyopewa na WBF ambayo inamtaka Cheka ashinde pambano hilo ili aweze kuwania ubingwa wa Dunia hapa hapa nchini.

error: Content is protected !!