October 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

CHAVITA waishushia tuhuma NEC

Spread the love

CHAMA cha watu wenye ulemavu wa kusikia nchini (Chavita) kimelalamikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutowaandalia mazingira mazuri wakati wa kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu uliofanayika Oktoba 25 mwaka huu, Anaandika Faki Sosi …(endelea).

Malalamiko hayo yametolewa leo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dickson Mveyange alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mveyange amesema kuwa, jumla ya watu 709 wasiosikia hawakupiga kura kutokana na NEC kutoandaa wasimamizi walio na ujuzi wa kuzungumza lugha za alama.

Mveyange amesema kuwa changamoto zilianza wakati wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumau la wapiga kura (BVR) ambapo watu 2,516 wenye ulemavu huo walijiandikisha na kwamba ni idadi ndogo kwa watu wenye ulemavu nchini.

Ametaja changamoto walizokutana nazo walemavu hao kuwa ni pamoja na wasimamizi kuwahoji maswali yasiyokuwa ya msingi pamoja na kuwakemea kwa sauti ya juu licha ya wao kutokuwa na uwezo wa kusikia hivyo kutafsiriwa kama manyanyaso.

Amesema NEC haikuandaa utaratibu mzuri kama kuweka vitambulisho vya kuwatambulisha, kuwaandalia watu maalim wa kuwasaidia hivyo walilazimika kukaa kwenye foleni kama watu wengine.

Mveyange amesema kuwa, tume pia haikushirikisha chama hicho kwenye utoaji wa elimu ya kiraia na upigaji kura hivyo ametoa rai kwa NEC kuandaa mazingira rafiki kwa walemavu kipindi cha chaguzi.

error: Content is protected !!