January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CHAVITA kuadhimisha ya wiki Viziwi Duniani

Spread the love

CHAMA Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kupitia tawi la Mkoa wa Pwani wapo katika Maadhimisho ya wiki ya viziwi duniani ambayo yameanza Agosti 21 na kumalizika Agosti 27 mwaka huu, kwa Tanzania hufanyika Kibaha mkoani Pwani. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Jinsia na Maendeleo CHAVITA, Lupi Mwaisaka Maswanya, kupitia mkalimani wake amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kujenga mwamko wa jamii kutambua rasmi lugha za alama kama njia ya mawasiliano.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Kwa Haki za Lugha ya Alama ya Tanzania, Watoto Wetu Wanaweza”.

Amesema kuwa jamii kujua lugha hiyo itasaidia viziwi kupata taarifa za msingi na kujadili na kushiriki katika midahalo mbalimbali ya kimsingi.

Amesema kuwa wadau wengine ambao ni asasi zote zinazotoa huduma kwa viziwi, shule za viziwi, wazazi wa viziwi, wasanii viziwi Hospitali ya Ccbrt, Shirikisho la Vyama Vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA).

Maswanya amesema kuwa, utambuzi wa lugha hizo kwa jamii itasaidi watoto viziwi kupata elimu, kukuza vipaji na kushiriki katika kusimamia ndoto zao.

Aidha amesema kuwa hawapati kujua sera za wagombea kuelekea uchaguzi mkuu wa kuamua kiongozi gani anayefaa kuwaongoza na kuongoza taifa kwa kukosa wataalumu wa alama katika majukwa ya kisiasa na kutopata elimu ya kiraia wayopaswa kupewa na serikali.

Maadhimisho hayo yaliamuliwa nchini Italia katika mji wa Roma Septemba 1951 na kuanza kuadhimishwa rasmi mwaka 1958 ambako hufanyika katika wiki za mwisho za mwezi Septemba.

error: Content is protected !!