July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chauma wamvaa Jaji Mtungi

Spread the love

MAKAMU Mwenyekiti Chauma Taifa, Kayumbo Kabutari, amemshukia msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mtungi kwa kumtaka atoe tamko ni kwanini vyama vya siasa vya upinzani vinazuiliwa kufanya mikutano.

Akizungumza na MwanaHALISI Online  katika mahojiano maalumu juu ya zuio la kutofanyika mikutano ya kisiasa Kabutali amesema ni hujuma zinazofanywa na msajili wa vyama vya siasa.

Amesema msajili wa vyama vya siasa nchini ndiye msimamizi na mlezi wa vyama hivyo hivyo kitendo cha serikali kupinga kuwepo kwa mikutano ya siasa na msajili akanyamaza ni dalili za kushindwa kutekeleza majukumu yake.

“Kitendo cha serikali kuzuia mikutano ya kisissa ni kuvunja sheria za nchi kwa mujibu wa sheria ya nchi katiba, sheria Na.5 ya mwaka 1992 ya sheria ya vyama vya siasa.

“Pia kuna sheria Na.32 yenye marekebisho ya mwaka 1994 ambayo inaruhusu vyama nya siasa chini na mfumo wa vyama vingi kufanya mikutano na maandamano huku wakiwa wametoa taarifa jeshi la polisi,” ameeleza Kabutali.

Kutokana na hali hiyo Kayumbo amemtaka Jaji Mtungi kutoa tamko kama anafanya kazi yake kwa mujibu wa sheria na kanuni za msingi wa vyama vya siasa au anaendeshwa na serikali iliyopo madarakani.

Amesema kwamba inasikitisha kuona mwanasheria tena Jaji ambaye ni msimamizi na mlezi wa vyama vya siasa ananyamaza na serikali inaendelea kuminya uhuru wa demokrasia.

“Haiwezekani sheria inaruhusu kufanya mikutano na maandamano kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi leo hii serikali inazuia kama ni hivyo basi wapeleke sheria hiyo Bungeni ili ifutwe na ijulikane kama siasa za nchii hii ni za Chama kimoja,” amesema Kabutali.

error: Content is protected !!