August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chaso wachangia damu Dodoma

Wananchi wakichangia damu salama

Spread the love

UMOJA wa Wanafunzi wa  Chadema Vyuo Vikuu  (CHASO) Mkoa wa Dodoma wamejitokeza kupokea wito wa kuchangia damu salama zaidi ya chupa 50, anaandika Dany Tibason.

 Zoezi hilo lilifanyika juzi wakati wa maadhimisho ya kilele uchangiaji damu salama duniani ambayo ufanyika Juni kila mwaka.

Akizungumza  na waandishi wa habari katika tukio hilo lililoambatana na usafishaji wa mazingika katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Dodoma, James Chindengweke Katibu Mwenenzi wa Chaso Mkoa , alisema umoja huo umejitokeza katika uchangiaji wa damu ili kuokoa maisha ya watu wengine walioko hospitalini husani akina mama na watoto pamoja na wale wanaopata ajali.

Alisema pamoja na uchangiaji huo pia wametumia maadhimisho hayo kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye maeneo mbalimbali ya manispaa ikiwemo na Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma.

Chindengweke alisema suala la kutoa damu siyo suala la kiitikadi kutokana na kwamba suala la uhitaji wa damu ni la kila mmoja na binadamu wanaunganishwa kwa damu.

Mbali na hilo alisema wasomi  pamoja na jamii kuendelea kuchangiaji huo wa damu na kuondoa hofu kuwa ukitoa unaweza ukapatikana na magonjwa.

“Hakuna haja ya kuhofia katika zoezi hili la utoaji damu ukizingatia kuwa utoaji huo umekuwa ukiwasaidia jamii mbalimbali yenye uhitaji damu pindi inapokosekana kwenye mwili”alisema.

Naye Kaimu Katibu wa Chaso Mkoa wa Dodoma Theodor Hango alisema vyuo vilivyoshiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu na ufanyaji wa usafi wa mazingira ni pamoja na Chuo cha Elimu ya Biashara,(CBE) Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Chuo cha Mipango, na St John.

Hango pia aliwataka  waataalamu wa afya kutokuwa sababisho la vifo vya watu kutokana na kukosa huduma ya afya kwa kuifanya kama sehemu ya biashara.

Kwa upande wake mwanafunzi wa chuo cha Udom  Erney Kawa ameitaka serikali kutoa elimu kwa jamii ili waweze kujitolea uchangiaji wa damu ukizingatia kuwa vifo vingi vinatokea kwa watoto na wanawake kutokana na hospitali zilizo nyingi kukosa damu.

Alisema elimu hiyo ikiwa itatolewa wengi wataondokana na hofu ya kutochangia utoaji wa damu ,hivyo ni muhimu serikali kwa kutumia wataalamu wake kupeleka elimu hiyo ili zoezi hili liweze kufanikiwa badala ya kusubiri kwenye maadhimisho.

error: Content is protected !!