January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Charles Hilary ateuliwa Ikulu Z’bar

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi amemteua mtangazaji mkongwe nchini, Charles Hilary kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano Ikulu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Hilary alikuwa mtangazaji wa Azam Televisheni, ameteuliwa leo Alhamisi, tarehe 30 Desemba 2021 kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Abdul Van Mohamed aliyekwenda masomoni nchini Uingereza.

Hilary amewahi kufanya kazi Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo sasa ni
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Redio One na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Katika uteuzi mwingine uliofanywa na Rais Mwinyi, amemteua Yusuph Majid Nassor kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBC) na Dk. Idrissa Muslim Hija kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uhaulishaji Ardhi Zanzibar.

error: Content is protected !!