August 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Charles Boniface Mkwasa Katibu Mkuu Yanga

Aliyekua Kocha Mkuu wa timu ya Taifa 'Taifa Stars' Charles Boniface Mkwasa

Spread the love

ALIYEKUA kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Charles Boniface Mkwasa ametangazwa kuwa katibu mkuu wa klabu ya Yanga, baada ya kumaliza mkataba wake na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF).

Kabla ya Mkwasa kuwa kocha muu wa timu ya taifa alikuwa kocha mkuu msaidizi wa wa Yanga chini ya Hans Van Plujim ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa benchi la ufundi wa klabu hiyo .

Mkwasa ameenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Dr Jonas Tiboroha ambaye aliondoka klabuni hapo na nafasi hiyo ilikuwa imekaimiwa na naibu katibu mkuu Baraka Deusdedit kwa kipindi cha muda mrefu mpaka uteuzi mwengine ulipofanyika leo.

Toka alipokuwa kocha wa timu ya Taifa, tangu Julai mwaka 2015 baada ya kurithi nafasi ya Mholanzi, Mart Nooij na katika kipindi chake aliiongoza timu hiyo katika mechi 13, ikishinda mbili, kufungwa sita na sare tano.

error: Content is protected !!