May 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chanzo ajali ya Chadema hiki hapa

Spread the love

GARI lililowabeba baadhi ya maofisa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kupata ajali katika eneo la Msoka, Kata ya Ngogwa iliyopo kwenye Jimbo la Masalala, Shinyanga ni kupasuka kwa matairi mawili ya gari. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Gari hilo lililokuwa  kwe nye msafara wa Salum Mwalimu, m gombea mwenza wa Tundu Lissu (Chadema) lililowabeba maofisa wane wa chama hicho, lilianguka na kuharibika vibaya jana tarehe 21 Septemba 2020. Hata hivyo, hakuna aliyefariki dunia.

Akizungumza na mtandao huu leo tarehe 22 Septemba 2020, Gerva Lyenda, Katibu wa Salum amesema, chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa matairi ya gari ya upande wa kulia.

Amesema, gari hiyo haikuwa mwendo wa kasi, na kwamba watu wote waliokuwamo katika gari hiyo wametoka salama.

“Tairi la nyuma ilipasuka na ya mbele ikafuatia kupusuka. Zote za upande wa kulia, gari haikuwa mwendokasi, tulikuwa wanne ndani lakini hatujaumia, tulitoka salama,” amesema Lyenda.

Lyenda amesema, asubuhi ya leo wapo kwenye maandalizi ya kwenda hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya, kisha jioni wanaendelea na kampeni.

“Hatujajua kama tumeathirika kwa ndani. Tunajiandaa kwenda hospital ili kufanya vipimo vya afya,” amesema Lyenda bila kutaja jina la hospitali wanayotarajia kwenda.

Ajali hiyo ilitokea majira ya jioni wakati Msafara wa Mwalimu ukitoka kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Msalala, wakielekea kwenye mkutano mwingine wa kampeni wilayani Kahama.

error: Content is protected !!