August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Channel Ten yawekwa kiporo

Neville Meena, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania

Spread the love

JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF) limekiweka kiporo kituo cha Televisheni cha Channel Ten kwa kukiuka makubaliano ya kutoandika wala kutangaza habari zinazomuhusu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, anaandika Hamisi Mguta.

Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena leo ameeleza kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari amesema TEF inakiri kutangazwa kwa habari za Mkuu wa mkoa huyo zaidi ya mara moja na imekuwa kawaida kwa vyombo vya Sahara Media (Star TV na Radio Free Afrika) kwa kuzingatia kwamba kufanya hivyo ni kukiuka makubaliano na mshikamano wa kitaaluma.

“Uongozi wa Jukwaa unalifanyia kazi hili ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na taasisi husika na baadaye utatoa taarifa rasmi kuhusu matokeo ya mchakato huo, kwasasa tunawakumbusha wahariri na waandishi kwamba makubaliano yetu ya kutotangazwa kwa habari zozote zinazomuhusu Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bado yapo palepale,” amesema Meena.

Aidha amesema aliyefungiwa kutotangazwa habari zake ni Mkuu wa mkoa na si habari za mkoa  wa Dar es Salaam hivyo habari zinazohusu matatizo, changamoto na maendeleo na maendeleo ya wananchi zinaweza kuandikwa.

 

error: Content is protected !!