Sunday , 5 February 2023
Home Kitengo Maisha Afya Chanjo ya Korona kuanza Agosti 3, vituo 550 kutumika
AfyaTangulizi

Chanjo ya Korona kuanza Agosti 3, vituo 550 kutumika

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi
Spread the love

 

WIZARA ya Afya nchini Tanzania, imesema huduma ya chanjo ya Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19), itaanza kutolewa kwa wananchi kuanzia Jumanne, tarehe 3 Agosti 2021, katika mikoa ya Tanzania Bara. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 30 Julai 2021 na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Prof. Abel Makubi, akitangaza vituo vitakavyotumika kutoa chanjo hizo.

Prof. Makubi amesema kuwa, chanjo hizo zitaanza kutolewa kwa makundi yenye uhitaji mkubwa, ambayo ni, watumishi wa sekta ya afya, watu wazima kuanzia umri wa miaka 50 na kuendelea na watu wenye magonjwa.

“Kutokana na mwongozo wa chanjo wa Taifa dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19, ule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), maelekezo ya Covax Facility na upungufu wa uzalishaji wa chanjo toka viwandani, chanjo hizi kwa sasa zinatolewa kwa kufuata vipaumbele vya makundi yenye uhitaji mkubwa,” amesema Prof. Makubi.

Katibu mkuu huyo wa wizara ya afya, amesema vituo takribani 550 vitatumika kutoa huduma hiyo, katika mikoa yote Tanzania Bara.

“Serikali inategemea kutoa chanjo kwa makundi yanayolengwa, kuanzia tarehe 3 Agosti 2021, siku ya Jumanne, katika vituo 550 vya kutolea huduma katika mikoa yote ya Tanzania Bara,” amesema Prof. Makubi.

Prof. Makubi amesema, walengwa wanapaswa kwenda katika vituo hivyo wakiwa na kitambulisho.

“Wananchi wanatakiwa kujihakiki kama wapo ndani ya makundi matatu ya walengwa kwa sasa. Kuandaa kitambulisho cha kazi, kitambulisho cha Taifa (NIDA)na cha kupigia kura, leseni ya udereva, pasi ya kusafiria au kitambulisho chochote kinachotambulika kisheria,” amesema Prof. Makubi.

Prof. Makubi amesema, wananchi watakaotaka kuchanjwa, wanapaswa kujisaliji mapema “wanatakiwa kufanya “booking” ya siku ya kuchanjwa kwa kutumia mtandao ndani ya simu au kompyuta yako kupitia au kwa kwenda moja kwa moja kwenye kituo na kujisajili kuanzia Jumatatu tarehe 2 Agosti 2021pamoja na kujaza fomu ya uhiari wa kuchanjwa.”

Serikali ya Tanzania, ilipokea dozi 1,058,400 za chanjo yta Korona aina ya Johnson & Johnson, kutoka Serikali ya Marekani, kupitia mpango wake wa Covax, unaolenga kusaidia nchi zinazoendelea katika kukabiliana na janga hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Afya

Waziri wa Tamisemi apewa siku 14 afike Morogoro kutatua changamoto za Afya

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel...

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

error: Content is protected !!