May 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chanjo ya corona: WHO yaitenga Tanzania, Burundi

Spread the love

 

SHIRIKA la Afya duniani (WHO), limeiondoa Tanzania na Burundi katika orodha ya nchi za Afrika Mashariki zikazopewa chanjo ya virusi vya corona (COVID-19). Inaripoti BBC…(endelea).

Taarifa zinaeleza, chanjo (dozi) milioni 336 za AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech, zitatolewa kwa muhula wa kwanza na wa pili wa mwaka 2021.

Nchi ambazo zitanufaika na chanjo hiyo ni Kenya (dozi 4,176,000), Rwanda (dozi 1,098,960), Sudan Kusini (dozi 864,000) na Uganda (dozi) 3,552,000. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ipo kwenye orodha hiyo.
WHO limetangaza mpango wa muda kuhusu na namna nchi hizo zitakavyopatiwa ili kujikinga na maambukizi ya corona.

Kwa awamu hii, nchi hizo zitapatiwa chanjo kwa idadi ya asilimia ya watu 3.3 kwa kila nchi, ni kutokana na malengo ya shirikisho la chanjo duniani (GAVI), ya utoaji wa chanjo kwa asilimia tatu ya wakazi dunia ndani ya miezi sita ya kwanza ya mwaka 2021.

Mataifa mengine ambayo hayatopewa chanji na WHO ni Equatorial Guinea, Eritrea, Gabon, Lesotho, Madagascar na Ushelisheli.

Wiki iliyopita Rais wa Tanzania, John Magufuli aliitahadharisha Wizara ya Afya kutopokea chanjo za corona, aliitaka wizara hiyo kuwa makini.

WHO imeeleza sababu ya kutojumuisha nchi hizo kwenye mpango wake wa chanjo ni kutokana na zilijinunulia chanjo zake zenyewe na hazikuomba au hazimo katika orodha ya nchi zitakazopewa chanjo.

error: Content is protected !!