May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chanjo ya corona kuingia Tanzania

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imeruhusu kuingizwa nchini, chanjo ya corona, miezi mitatu baada ya aliyekuwa rais wake, John Magufuli, kufariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerison Msigwa, hatua hiyo inajiri baada ya mrithi wa Dk. Magufuli, Rais Samia Suluhu Hassan, kuunda tume ya ushauri na kupokea mapendekezo ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika kipindi cha utawala wa Magufuli, ugonjwa wa corona ulionekana kama hauwahusu wananchi wa Tanzania.

Kufuatia uamuzi huo, raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki, sasa watakuwa na fursa ya kupata chanjo ya corona nchini humo.

Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Rais amesema, balozi na taasisi za kimataifa zimeruhusiwa kuingiza chanjo nchini, ili kuwachanja raia na watumishi wake, kuendana na taratibu za nchi hizo.

Amesema, watumishi hao wamekuwa wakipata kadhia mbalimbali katika utendaji kazi wao wa kazi, kutokana na kushindwa kupata chanjo hiyo.

Hata hivyo, Rais Samia amesisitiza kuwa chanjo hizo zitaletwa nchini mwake, kwa utaratibu utakaoratibiwa na wizara ya afya.

Rais aliamua kuunda kamati ya wataalamu kwa lengo la kuishauri serikali kuhusu mwelekeo wa kukabiliana na janga hilo.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Dorothy Gwajima

Alichukua hatua hiyo, muda mfupi baada ya rais Samia kuchukua madaraka kutoka kwa Dk. Magufuli.

Katika mapendekezo hayo, kamati imeishauri serikali kuhusu njia mbalimbali itakazotumia kupata fedha ndani ya bajeti ya serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo yakiwemo mashirika ya kimataifa kwa ajili ya kugharamiakia vifaa, tiba mafunzo na chanjo.

Kwa upande wake, rais Samia ameipongeza kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Profesa Said Aboud kwa kazi nzuri na kumuagiza waziri wa Afya bi Dorothy Gwajima kuandaa andiko litakalowasilishwa kwa baraza la mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa kabla ya serikali kufanya maamuzi kuhusu mapendekezo hayo.

error: Content is protected !!