January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Changamoto mpya 2045: Uhalifu kwa kutumia vishada na Vinasaba

Picha ya mharifu wa mitandao

Spread the love

NI changamoto gani tutakumbana nazo hapo mwaka 2045? Hili ni swali linalogonga vichwa vya walimwengu kwa sasa.

Katika kujibu swali hili, kikundi cha magwiji wa jeshi la Uingereza wametabiri kuwa ifikapo mwaka 1945 “kutakuwepo mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, upelelezi wa hali ya juu, majeshi ya mashirika, silaha za kisasa wenye uwezo wa kushambulia kwa kulenga vinasaba (DNA) na magaidi wenye uwezo wa kutengeneza virusi hatari.

Majibu hayo yapo ndani ya ripoti iliyoandaliwa na Wizara ya Ulinzi ya Uingereza. Ripoti hiyo inasema katika kipindi cha miaka 30 ijayo, idadi ya watu duniani itazidi bilioni 9. Uwepo wa maendeleo ya teknolojia na mabadiliko ya mambo mengine yataibadilisha kabisa dunia na kuleta hofu.

Kwa mujibu hati hiyo inayoitwa Global Strategic Trends by the Development, Concepts and Doctrine Centre. Hatari zinazotabiriwa ni pamoja na miji iliyoshindwa na miji inayoendelea kushindwa kusababisha hatari kubwa ya usalama wa mataifa, uongezekaji wa mafuriko na ukame kwa baadhi ya maeneo hivyo kusababisha uharibifu mkubwa na vifo.

Tatizo lingine litatokana na ukuaji wa miji, hasahasa chini ya jangwa la Sahara. Watu zaidi ya bilioni 3 wataishia kuishi kwenye makazi duni (slums) kwa miongo 3 kama hakutakuwa na uwekezaji katika huduma muhimu na miundombinu. “Maeneo haya hayatakuwa na utulivu wa jamii, “ hati hiyo ilitamka.

Ongezeko la ushushushu na hofu ya mashambulizi ya mitandao

Utafiti huo ulisema wakati habari, mawasiliano, na miundombinu muhimu ya mataifa imeweza kuunganishwa kirahisi kwa kutumia teknolojia, kuna uwezekano wa kuongezeka kwa tishio la uharibifu wa miundo ya mitandao na wizi wa taarifa nyeti kutoka kwenye mitandao utakaofanywa na waalifu na magaidi utafiti huo ulisema.

Mfano mfumo wa usafirishaji unaweza ukawa ni sehemu inayolengwa kwa waalifu hao.

“Kuongezeka kwa vifaa vyenye uwezo wa kukusanya taarifa kunasbabisha ongezeko la upelelezi na ushushushu. Vyombo vyenye uwezo wa kuficha taaarifa vitazidiwa na kutokuwa na sifa hiyo ya utunzaji wa siri. Wataalamu wa ubunifu wa IT watakuwa na changamoto kubwa,”utafiti huo ulisema.

Kuongezeka kwa ndege zisizotumia watu vishada (drones) na satelaiti (vifaa ambavyo siku za karibuni vimeweza kupatikana kwa gharama ndogo) kutapelekea wahalifu na magaidi kujenga uwezo wa kuvitumia na kuvimiliki.

Uchunguzi huo umetabiri kuwa kufikia mwaka 2045 au kabla ya hapo , mashirika ya kihalifu yanaweza kumiliki roketi zitakazokuwa zinaendeshwa na makampuni binafsi – hii itawaruhusu kuanzisha satelaiti zao za uchunguzi, na hivyo kutishia haki ya kutoingiliwa ya mtu binafsi au makampuni.

Watumiaji wakubwa wa fedha kwa vifaa vya kijeshi Marekani na China watakuwa juu ya mataifa mengine na inakisiwa matumizi yao yatafikia 45% ya gharama za vifaa vya kijeshi duniani. Inasemekana India itakuwa na gharama za kijeshi zinazofanana na bajeti za kijeshi nchi zote za Ulaya.

Kwa vile vitambuzi vya kijeshi (military sensors) vinaendelea kuwa vya kisasa (sophisticated) zaidi na vimesambaa kwa wingi, shabaha na usahihi wa utunguaji utaongezeka hivyo kufanya ugumu wa watu au vifaa kufichwa bila kutambulika.

Vifaa hivi vitakuwa na uwezo mkubwa kiasi kwamba vinaweza kumdhuru mtu kwa kutumia sahihi ya digitali aliyonayo (digital signature) au kutumia vinasba (DNA) vyake. Hii itasaidia watunguaji kumlenga mtu mmoja tu kwenye kundi la watu wengi.

Pia tutaona vita ya kisasa kabisa ya mazingira, vita yenye uwezo wa kueneza magonjwa kwa wanadamu kwa kutumia wadudu au mashine zenye wadudu waliotengenezwa kwa kubadilishwa. Utafiti huu umetabiri kuwepo na mlipuko wa vitambi na magonjwa ya akili.

Serikali za kidikteta, magaidi na wahalifu watapata nafasi ya kutengeneza vijidudu vyenye uwezo mkubwa wa kuambukiza na virusi hatari sana kama silaha ili kuweza kutimiza matakwa yao ya kisiasa na kiitikadi.

“Inawezekana pia virusi vitatengenezwa kwa siku zijazo ili kuangamiza watu Fulani, kundi fulan I la watu kama silaha muhimu sana” . Utafiti huo umeonyesha.

Kwa upande wa mafanikio yaliyooneshwa kwenye ripoti hiyo, waandishi wametabiri na kusema wanashukuru maendeleo na uboreshaji kwa upande wa utabibu kwani siku za kuishi zitaongezeka.

Hata hivyo ukosefu wa ushughulishaji mwili kwa mazoezi, ulaji wa vyakula visivyojenga mwili, kuna tishio linguine hapa la mlipuko wa watu kunenepena, kuwa na vitambi, na kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukiza kama vile kupoteza uwezo wa ubongo kuwa na kumbukumbu, kufikilia na kutoa maamuzi.

error: Content is protected !!