
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe akiwa Chamwino akisaka wadhamini
WANANCHI wa kijiji cha Chilangali Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma ,wametakiwa kutoichagua CCM katika uchaguzi mkuu ujao kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kufuga nyoka katika gunia la unga. Anaandika Dany Tibason … (endelea).
Mbali na kuhimizwa kutoichagua CCM wananchi hao wameelezwa sababu za kuwa masikini ikiwa CCM ni moja wapo ya sababu za wananchi kuendelea kuwa masikini wa kutupwa licha ya taifa kuwa na rasilimali nyingi.
Aidha,wameelezwa kuwa umasikini unaowakabili wananchi unatokana na uongozi mbovu wa serikali iliyopo madarakani kwa kushindwa kutumia rasilimali za nchi kuondoa umasikini na badala yake serikali hiyo imetengeneza matabaka kwa walionacho na wasionacho.
Kauli hiyo ilitolea na mtangaza nia ya kuwania ubunge kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema), John Chigongo ambamo anagombea ubunge katika jimbo la Chilonwa Wilaya Chamwino Mkoani hapa.
Amesema kuwa kijiji cha chilangali ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na tatizo la huduma za afya ambapo huduma inayotolewa katika zahanati ni dumi.
Aidha,amesema Chogongo alisema kuwa zipo shule nyingi za sekondari zimeanzishwa katika jimbo hilo na wanafunzi wengi huioshia kidato cha nne ambapo husababishwa na serikali kutoweka sera za kutosha.
Nae Mkurugenzi wa Oganaizeisheni na mafunzo na Usimamizi wa Kanda, Benson Kigaila amewataka watanzania kuwa kama kocha wa timu ambaye akihonga mchezaji hachezi kwa kiwango kinachotakiwa anamuweka benji anamuingiza mwingie kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanashinda.
“Watanzania fanyeki kazi ya kuangalia kama chama kimeshindwa kufanya kazi king’oeni muweke kingine ambacho mtaona kutawaletea mabadiliko ya kweli katika eneo husika, usibaki kung’ang’ania kile kile badilisha kingine muone,” amesema Kigaila.
More Stories
Sakata la Mahindi Kenya Vs Tanzania: Zitto aonesha njia
COVID-19: Prof. Lipumba ‘watu wana hofu’
CCM ya tetea wazawa miradi ya ujenzi