January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chama uso kwa uso na Simba, kombe la Shirikisho

Spread the love

 

Clatous Chama Raia wa Zambia akiwa na kikosi cha RS Berkane atakutana uso kwa uso na timu yake ya Zamani ya Simba kwenye mchezo ya hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho Barani Afrika kufuatia kupangwa kundi moja. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Timu hizo mbili zimepangwa kundi D, sambamba na Asec Mimosa kutoka Ivory Coast na US Gendarmerie Nationale ya Nigeria mara baada ya kuchezeshwa droo hii leo.

Chama anakutana tena na waajili wake wa zamani ikiwa imepita miezi mine toka alipoachana nao na kujiunga na RS Berkane ya nchini Morocco kwenye dirisha kubwa la usajili sambamba na winga wa klabu ya Yanga, Tuisila Kisinda.

Mchezaji huyo aliondoka ndani ya klabu ya Simba huku akiwa na m,afanikio makubwa ikiwa kuipeleka timu hiyo hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya Mabingwa mara mbili na kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ikumbukwe RS Berkane kwa sasa inanolewa na Florence Ibenge kocha wa zamani wa klabu ya AS Vita ya nchini Congo.

error: Content is protected !!