May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chama, Onyango ‘out’ dhidi ya Namungo

Clatous Chama, kiungo wa klabu ya Simba

Spread the love

 

Wachezaji watatu wa klabu ya Simba Josh Onyango, Clatous Chama na Ame Ibrahim watakosekana kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Namungo kocha msaidizi wa klabu hiyo Seleman Matola amethibitisha. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo namba 143 utachezwa kesho kwenye Uwanja wa Majaliwa uliopo Ruangwa, Lindi ambao ni wa mzunguko wa kwanza.

Akiongea na waandishi wa Habari hii leo Matola amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo huo isipokuwa Josh Onyango, Clatous Chama na Ibrahim Ame.

“Tutakosa huduma ya Onyango ambaye bado afya yake haijaimarika vizuri, Chama ameaga ana matatizo ya kifamilia na Ame anayetumikia adhabu ya kufungiwa.” Alisema Matola

Josh Onyango, Beki wa Simba

Simba imesafiri hii leo kutoka jijini Dar es Salaam wakiwa na msafala wa wachezaji 20.

Aidha katika hatua nyingine kocha huyo alinena kuwa wameenda mkoani Lindi kutafuta pointi tatu licha ya kukili kuwa Namungo FC ni timu nzuri hasa wanapokuwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani na mchezo utakuwa mgumu.

Ibrahim Ame, beki wa kati wa Simba

“Tunamshukuru Mungu tumefika salama hapa Lindi, wachezaji wote wako vizuri. Tunajua haitakuwa mechi rahisi Namungo ni timu nzuri hasa inapocheza nyumbani lakini sisi tumejipanga kuondoka na alama zote,” amesema Matola.”Aliongezea Matola.

error: Content is protected !!