May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chama mchezaji bora mwezi Aprili

Clatous Chama

Spread the love

 

KIUNGO wa timu ya Simba Clatous Chama amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mashabiki wa klabu hiyo wa mwezi Aprili mara baada ya kuwashinda Shomary Kapombe na Aishi Manula. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezaji huyo ametangazwa hii leo kupitia kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Katika kinyang’anyiro hiko Chama alipaka asilimia 50.48 za kura zote huku Aishi Manula akipata asilimia 30.74 na Shomari Kapombe akipata kura asilimia 18.78

Chama anakuwa mchezaji wa tatu kushinda tuzo hii toka zilipoanza kutolewa mwezi Februari ambapo mshindi alikuwa Luis Miquisson na mwezi Machi tuzo hiyo ilinyakuliwa na beki wa kati Josh Onyango.

error: Content is protected !!