MABINGWA watetesi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba imesema katika mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya watani zao Yanga watakosa huduma ya kiungo wao, wao Clatous Chama, Bernard Morrison na Meddy Kagere. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)
Chama aliumia katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) 2020/21 uliochezwa Jumatano ya tarehe 4 Novemba 2020 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Simba iliibuka na ushindi wa 2-0. Magoli hayo yalifungwa na nahodha John Bocco kwa penati na Hamis Ndemla aliyepokea pasi ya Chama.
Chama ambaye ni raia wa Zambia hakumaliza mchezo huo baada ya kuumia kwenye mchezo huo na kutoka dakika ya 69 na nafasi yake kuchukuliwa na Miraji Athuman.

Simba itamkosa Morrison ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mitatu, huku Kagere na Gerson Fraga wakiwa majeruhi baada ya kuumia katika michezo iliyopita.
Kocha Mkuu wa Simba, Seven Vandenbroeck akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa tarehe 6 Novemba 2020 amesema, katika mchezo wa kesho Chama hatakuwemo kwenye mipango yake.
Wakati Seven akiwakosa nyota wake hao ambao wamekuwa tegemeo katika kikosi cha kwanza, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema, yeye atawakosa nyota wake Haruna Niyonzima anasumbuliwa na malaria, Mapinduzi Balama na Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ ambao ni majeruhi.
Leave a comment