CHAMA cha Wapangaji Tanzania (Tanzania Tenants Association), kimeiomba serikali kuweka chombo maalum kwa ajili ya kulinda maslahi ya wapangaji, anaandikaCatherine Kayombo.
Akizungumza na wanahabari, katibu mkuu wa chama hicho, Ndumey Mukama amesema kuwepo kwa chombo hicho kutasaidia kusimamia sheria ya upangaji nchini ikiwemo ulipaji wa kodi kulingana na mandhari na hadhi ya nyumba husika.
“Kuwepo kwa mamlaka hii kutasaidia kusimamia na kuhakikisha kuwa hakuna mabadiliko ya viwango vya kodi za pango yasiyozingatia hali ya nyumba ya eneo husika na mwenendo wa soko” ,amesema Ndumey.
Katibu mkuu huyo pia ametoa rai kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi kuweka sera ya nyumba ili kusaidia kutoa mwongozo wa mwenendo wa suala la upangaji na kuweka mkakati utakaosimamiwa na serikali.
Aidha, uongozi huo umetaka udalali wa shughuli za upangishaji uzuiwe kisheria, na kutaka chama kipewe ridhaa ya kufanya hivyo kupitia chama chao.
Leave a comment