January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chama cha Cameron chashinda tena Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron

Spread the love

DAVID Cameron, ataendelea kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya chama chake cha Conservative (Tory) kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 7 mwaka huu, katika ushindi ambao haukutarajiwa.

Ushindi huu ni kinyume na utabiri uliofanywa awali na vyombo vya habari pamoja na kura ya maoni iliyofanywa na wananchi. Maoni ya wengi yalionyesha kuwa vyama hivyo vikubwa vya Labour na Conservative kuwa sare.

Huku maoni mengine ya viongozi wa Tory wenyewe yakionyesha kuwa watapata sio zaidi ya viti 290 na hamna ambaye aliongelea kuweza kupata viti 300 na zaidi, hivyo kuwaweka katika nafasi ya kufikiria kuunda serikali ya mseto.

Utabiri uliopita ulionyesha hamna chama kitakachoweza kupata ushindi wa moja kwa moja ili kuweza kuunda serikali bila ya kushirikisha chama kingine.

Conservative chini ya David Cameron kimepata ushindi mkubwa na hivyo tofauti na ushindi wake wa mwaka 2005 ambapo hakikuweza kuwa na idadi ya viti vinavyohitajika kuunda serikali na hivyo kulazimika kuunda serikali ya mseto na chama cha Liberal Democrats (Lib Demo).

Chama cha Cameron kimepata ushindi wa viti 331 kati ya viti 650 na hivyo kupata uhalali wa kuunda serikali. Ili kuweza kuunda serikali chama kinatakiwa kuwa na viti 326 (Majority Victory). Tory iliyopata jumla ya kura 11,334,920 imepata viti vipya 35 na kupoteza viti 11.

Uchaguzi huu ni pigo kubwa kwa chama cha Labour kinachoongozwa na Ed Miliband kilichofanya vibaya sana kwa kupata viti 232, kimepata viti vipya 22 na kupoteza viti 48, ikiwa viti 40 kati ya hivyo kimepoteza Scotland. Jumla ya kura ilizopata ni 9,347,326.

Pigo hili sio kwa Labour tu bali hata kwa wananchi waliochoshwa na sera la Conservative hasa wahamiaji walioathirika sana na sera za uhamiaji za serikali ya David Cameron zilizowabana na zenye masharti magumu.

Ed Miliband- Kiongozi wa Labour na aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Waziri Mkuu, amejiuzulu siku ya Ijumaa na amesema chama kinahitaji mtu mwingine wa kuweza kukijenga. “Ninajiuzulu baada ya usiku mgumu na wenye kupoteza matumaini,” amesema.

Akiongea kutoka London kwa njia ya simu, Milaband alimpongeza Cameron kwa ushindi

Aliongeza: “Uingereza inahitaji Labour madhubuti. Uingereza inahitaji chama cha Labour kinachoweza kujiunda upya baada ya kushindwa. Kama tulirudi madarakani siku za nyuma, tutaweza kurudi tena siku zijazo”

Naye Nick Clegg kiongozi wa Lib Demo chama kilichoshika nafasi ya nne, amesema pia anajiuzulu, hii ni baada ya kupoteza viti 49 na kuambulia viti 8 tu.

Vyama hivi viwili ndio vyama vikubwa vyenye historia ya kubadilishana kwa kuwepo madarakani, kuanzia mwaka 80 mpaka 90 Tory ilikuwa madarakani kwa vipindi 3, ikaja Labour kwa vipindi vitatu 1995-2005, mwaka 2010 na 2015 chama cha Tory kimerudi madarakani.

Jumla ya wawakilishi 650 wamechaguliwa katika uchaguzo huo, uliohusisha watu milioni 50 waliojiandikisha.

error: Content is protected !!