Saturday , 20 April 2024
Home Kitengo Michezo Chama arejea Simba, atangazwa rasmi
MichezoTangulizi

Chama arejea Simba, atangazwa rasmi

Clatous Chama
Spread the love

 

KLABU ya soka ya Simba imetangaza rasmi kumrejesha kiungo wake raia wa Zambia Clatous Chama, mara baada ya kufanikiwa kumsajili tena akitokea kwenye klabu ya RS Berkane ambapo alivunja mkataba nao ara baada ya kudumu kwa miezi mitano. Anaripori Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Chama amerejea tena Simba kwa kusaini mkataba wa miaka miwili utakaomfanya adumu kwenye klabu hiyo hadi msimu wa 2021/22.

Mchezaji huyo amejiunga tena na Simba kwenye dirisha dogo la usajili akitokea RS Berkane inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco kufuatia kutopata nafasi ya kutosha ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza chini ya kocha Frolence Ibenge kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo toka alip[ojiunga nayo kwenye dirisha kubwa mwezi Agosti, 2021.

Uongozi wa Simba ulimfuatilia muda mrefu mchezaji huyo ambaye alihitaji mwenyewe kuvunja mkataba huo na kurejea nchini kwenye kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo alicheza kwa mafanikio.

Mchezaji huyo anakuja ndani ya klabu ya Simba kuchukua nafasi ya Duncan Nyoni ambaye klabu ya Simba imevunja mkataba nae kufuatia kutoonyesha kiwango kizuri miezi michache toka ajiunge na klabu hiyo.

Ikumbukwe Chama alifika nchini kwenye msimu wa 2018/19 na kucheza kwa mafanikio makubwa ndani ya klabu ya Simba akitokea nchini Zambia kwenye klabu ya Lusaka Dynamos.

Katika kipindi cha miaka mitatu Chama amefanikiwa kuipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu, Ubingwa wa kombe la Shirikisho mara mbili na kuifikisha hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

Michezo

Tusua mkwanja na mechi za Ijumaa leo

Spread the love  LEO hii mechi zinaendelea kote na wewe kama unataka...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!