May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chalamila amkingia kifua Hayati Magufuli

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya

Spread the love

 

ALBERT Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, amesema wanaojadili kwamba Hayati John Magufuli alikuwa dikteta, wanachosha akili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Chalamila ametoa kauli hiyo leo tarehe 19 Aprili 2021, wakati akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini katika Wilaya ya Chunya, mkoani humo.

Ametaka watu kutoingizwa kwenye mkumbo wa wale wanaosema, Hayati Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021, alikuwa dikteta katika utawala wake.

“Wengine nimesikia kwenye mijadala wanasema, Rais Magufuli alikuwa dikteta, ukimuona mtu anatokea sasa hivi anaanza kuongea wakati aliyekuwa Rais (Magufuli) amefariki, ujue huo ni mjadala hewa, msijiingize kwenye mijadala hiyo.”

“Ilifaa mumfikishie ujumbe wakati akiwa hai, mkianza kueleza mambo ambayo yeye amefariki, mnatuchosha akili,” amesema Chalamila akisitiza, mijadala inayoweza ‘kuwatoa kimaisha’ ni kuhusu kufanya kazi kwa bidii.

Chalamila amesema, watu hao walipaswa kumfikishia ujumbe Hayati Magufuli wakati akiwa hai kwamba yeye ni dikteta.

“Mijadala sahihi itakayotutoa kimaisha ni kazi, sio mijadala hewa…, mjadala wa kweli ni kuuliza umeme uko wapi? mbona barabara haijatengenezwa? mbona mawasiliano hakuna?

“Mjadala wa kweli nikusema hapa kuna watu wanatudai kodi wanatunyanganya kwa nguvu, tupate vituo vya afya vizuri, shule nzuri, tuwe na maisha bora. Mijadala hewa tuipotezee, haitatufikisha tunakokwenda,” amesema.

error: Content is protected !!