June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chakula cha sumu chauwa Watu 24 wa familia moja

Spread the love

 

WATU 24 wa familia moja wamefariki dunia nchini Nigeria, baada ya kula chakula chenye sumu. Inaripoti BBC … (endelea).

Taarifa ya tukio hilo imetolewa jana Jumanne na Kamishna wa Afya wa Jimbo la Sokoto, nchini humo, Ali Inname, akizungumza na waandishi wa habari.

Inname alisema, watu hao walikula chakula chenye sumu ya mbolea aina ya Gishirin Lalle, iliyowekwa katika chakula hicho kimakosa, wakidhani ni chumvi.

Kamishna huyo wa afya, alisema tukio hilo lilitokea Jumatatu, tarehe 9 Agosti 2021.

Hata hivyo, alisema wanafamilia wawili walinusurika kifo kwa kuwa hawakula chakula kingi. Watu hao wanapatiwa matibabu hospitalini.

Inname alishauri wananchi kutenganisha vyakula na vitu vyenye sumu.

error: Content is protected !!