Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko CHAKUA yazuiwa stendi ya Magufuli, Meneja afunguka
Habari Mchanganyiko

CHAKUA yazuiwa stendi ya Magufuli, Meneja afunguka

Spread the love

 

CHAMA cha Kutetea Haki za Abiria nchini Tanzania (CHAKUA), kimemlalamikia Meneja wa Kituo cha mabasi cha Magufuli, Mbezi jijini Dar es Salaam, Bakari Cheche kwamba amewazuia kufanya shughuli zao ndani ya stendi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Katibu Mkuu wa CHAKUA, Modest Nkurlu amesema leo Ijumaa, tarehe 7 Januari 2022, kuwa mwezi uliopita walikuwa na kikao na meneja wa kituo hicho cha mabasi cha Magufuli na kuwaagiza kwamba hawatakiwi kuonekana kwenye stendi hiyo.

Moja ya shughuli za CHAKUA ni kutoa elimu na kusimamia haki za abiria pale zinapovunjwa wakiwa katika mazingira ya safari.

Nkurlu a,edai meneja huyo aliwazuia kuendelea na shughuli zao kwa madai kwamba hawajui wanafanya nini, hawajui ni wakina nani na wamekuwa wasumbufu ndani ya stendi hiyo ya mabasi.

“Sisi tumesajiliwa kihalali na shughuli zetu zipo kisheria na kwa maslahi ya abiria. Kuna kampuni za mabasi, hazistahili hata kufanyakazi, CHAKUA tunapochukua hatua bila shaka wenye mabasi na wale wanaowalinda, hawaridhishwi ndio maana tunazuiliwa,” amesema.

Kwa mujibu wa Nkurlu, tayari wameandika barua kwenye mamlaka husika kulalamikia mwenendo wa Meneja wa kituo hicho cha mabasi na kusisitiza kuwa zuio lao ni kwa maslahi ya meneja huyo.

“CHAKUA tunafanyakazi katika standi zote nchi, Dodoma, Mwanza na meeneo mengine, lakini hatuzuiliwi, kwanini meneja wa kituo cha Magufuli anatuzuia,?” amehoji.

Akijibu malalamiko hayo, Cheche amesema hajakizuia chama hicho bali aliwataka viongozi wake waje na barua ya utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James.

Alisema chama hicho kipo kisheria, hawezi kukizuia, lakini waje na barua ya utambulisho kutoka kwa mamlaka husika ili ajue anafanyakazi na kikundi gani.

Alisema kuwa chama hicho kina mgogoro, hivyo alitaka kujua anafanyakazi na kikundi gani sahihi.

“Ndugu yangu, hawa watu walikuja, tumekaa nao ofisini, nilichowaambia ni kwamba waje na barua ya utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, tangu nilipowaagiza hadi leo ni zaidi ya mwezi, wanapata kigugumizi gani kuja,” amehoji Cheche.

Meneja huyo alienda mbali zaidi na kuhoji, “kama hapa kwenye stendi ya Magufuli nimewazuia, mbona pale kwenye stendi ya daladala ya Mbezi pia hawapo. Na hapo nimewazuia, kwanini wanang’ang’ania stendi ya Magufuli tu?,” alihoji.

Hivi karibuni CHAKUA, ilimsimamisha kazi Mwenyekiti wake taifa, Maulid Masalu, akisubiri uamuzi wa Mkutano Mkuu.

Uamuzi wa kumsimamisha Mwenyekiti huyo umetokana na mapendekezo ya kikao cha Kamati Tendaji ya CHAKUA iliyokutana kwa siku mbili, jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari Mchanganyiko

GGML yasisitiza kuendelea kuimarisha afya za wafanyakazi

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited kwa kushirikiana na kampuni...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

error: Content is protected !!