June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

CHAKUA chalaani uvunjwaji haki za abiria

Spread the love

CHAMA cha Kutetea Abiria Tanzania (Chakua) kimeiomba serikali kuhakikisha haki za msingi za abiria zinafuatwa na changamoto zao. Anaandika Regina Mkonde … (endelea).

Changamoto zinazoelezwa ni pamoja na adha ya usafiri, upangwaji wa nauli za usafiri kiholela, kutolipwa fidia abiria anapopata ajali na ubovu wa miundombinu kwenye baadhi ya vituo vya mabasi.

Chakua imetoa pendekezo serikalini la kutoruhusu nauli pendekezwa na Mradi wa Mabasi yaendao Kasi (DART) kuzidisha nauli za daladala kwani itashawishi daladala zingine kuongeza nauli kama za DART.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chakuaa kutoa msimamo wa nauli zao ambazo ziko juu ukilinganisha na nauli zinazotozwa kwenye daladala.

“Sumatra hawakutakiwa kujadili nauli za DART, pia hakuna sababu za msingi zitakazowafanya kupendekeza nauli za juu wakati sababu zinazotumika kupandisha nauli hazina mashiko kwa sasa,” amesema Mchanjama na kuongeza;

“Inafahamika kuwa, kupanda kwa mafuta, vipuli, kodi inaweza ikasababisha nauli kupanda. Lakini kwa sasa bei ya mafuta iko chini na kodi hazijapanda iweje nauli zilizopendekezwa ziwe juu, au kwa sababu mabasi ni mapya?” alihoji.

DART imependekezwa nauli ya ruti ndefu kutozwa kiasi cha shilingi 1400, kati 1200 na fupi 700 jambo ambalo linapingwa na serikali pia wananchi.

“Abiria wanateseka wakati wa usafiri, wanapanda daladala kwa shida, wanapangwa kama mihogo, kwa abiria wa mbali ikifika majira ya jioni wanapandishiwa nauli kiholela sababu ya uhaba wa daladala unaosababishwa na foleni. Tunaitaka serikali ihakikishe changamoto hii inatokomea.” amesema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Chakua, Modest Mfilinge.

Kutokana na adha ya usafiri, Serikasli imeombwa kutekeleza kwa vitendo tamko yake ya kila daladala kupakia abiria kulingana na uwezo wa siti zake ingawa wadau wengi wanapinga tamko hilo na kudai kuwa ni ngumu kutekelezeka.Lakini Chakua imesema kuwa inawezekana kukiwepo na mipango madhubhuti.

“Wadau wengi wanapinga utekelezwaji wa tamko la serikali la kila daladala kubeba abiria ‘level seat’ wakidai kuwa haiwezekani, hili linawezekana. Serikali inabidi ijue idadi ya daladala kwa kila barabara na ihakikishe zinafanya ruti,” amesema Mfilinge na kuongeza;

“Kama kuna barabara yenye daladala chache ziongezwe, daladala zinazo kata ruti zichukuliwe hatua kali za kisheria, wanaopandisha nauli kiholela wakati wa jioni wawajibishwe.

“Ijengwe miundombinu itakayosaidia kupunguza foleni. Kwa kufanya hivi tutafanikiwa kutekeleza tamko hili,” amesema Mfilinge.

Chakua imeitaka serikali kukikarabati kituo cha mabasi cha Ubungo ili kuondoa changamoto za usafiri zinazoewndelea kwenye kituo hicho na kuwa kutojengwa kwa kituo hicho, kumesababisha uwepo wa vitendo vya kihalifu.

error: Content is protected !!