January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chai, viazi almanusura vivunje semina ya walimu

Jumanne Sagini, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu (kulia) akifafanua jambo

Spread the love

WALIMU wakuu wa Shule za  msingi na Waratibu kata mkoani Mwanza, `alimanusura` wavunje  semina ya mafunzo ya uongozi wa elimu baada ya kunywa  chai na kiazi kimoja. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea)

Hali hiyo ilijitokeza  baada ya walimu hao kuona  washiriki wenzao wakikosa chai na waliobahatika  kunywa chai hiyo waliambulia kiazi kimoja na chai na kuamsha `sekeseke` hiyo iliyodumu kwa dakika 30.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao, walisema kuwa wengi wao wametoka wilayani lakini baada ya kuripoti kituoni hapo juzi hawajafahamu ni kiasi gani cha posho wanacholipwa.

“Mimi nimetoka sengerema nimefika hapa na leo tunaanza mafunzo lakini sijafahamu ni kiasi gani nalipwa, kama unavyoona mwenyewe  watu wamekunywa chai na kiazi kimoja, je posho yetu itakuwa kiasi gani,” alihoji.

Katika mshikemshike hiyo, Mmoja wa mratibu wa mafunzo hayo ambaye ni mkuu wa chuo cha uongozi wa elimu  Mkoa wa Mwanza, Benard Fundi, aliwaomba washiriki hao msahama na kwamba fedha zao za kujikimu watalipwa.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini,  amewaomba walimu wa Shule za msingi hapa nchini, kuacha kujihusisha na masuala ya siasa katika vituo vyao vya kazi.

Sagini amesema  watumishi wa umma hawaruhusiwi kujihusisha na masuala ya siasa  katika eneo la kazi na badala yake wanaweza kufanya siasa nje ya ofisi ili kulinda sheria na kanuni za watumishi.

Amesema  endapo mwalimu yeyote atekaegundulika na ushahidi ukaonekana anajihusisha na siasa ndani  ya eneo la kazi, atachukuliwa hatua stahiki na kuwa mfano kwa watu wa namna hiyo.

“Kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu, wapo walimu wengi ambao wanajihusisha na siasa ndani ya maeneo yao ya kazi,sasa natoa onyo kwa walimu wote wanaofanya siasa katika  eneo la kazi kuacha mara moja,” amesema Sagini.

Amewataka  walimu hao baada ya kumaliza mafunzo hayo, kufuatilia shughuli za ufundishaji na ujifunzaji kusoma na kuandika, upatikanaji wa takwimu za shule za msingi, kuongoza shule kwa ufanisi kwa kuzingatia utawala bora.

error: Content is protected !!