January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema:Pinda amepindisha ushauri wa Werema

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinamlalamikia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwa amepindisha ushauri wa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu, Jaji Fredrick Werema na hivyo kusababisha maafa ya wakulima na wafugaji wa vijiji vya Mbigiri na Mabwegere wilayani Kilosa, Morogoro. Anaandika Bryceson Mathias … (endelea).

Mwenyekiti wa Chadema kijiji cha Mbigiri, Maftaha Hamis, ameliambia Mwanahalisionline kuwa ni vizuri Pinda angezingatia uzuri wake, badala ya kupindisha ushauri huo.

Akionesha barua hiyo yenye kumb. Na. AGC/G.20/19162 ya Agosti 1, 2014, Hamis amsema “Jaji Werema alibaini uhalali wa Kijiji cha Mabwegere chenye usajili Na. 32758 wa 8.12.19, kwamba ulikuwa na shaka kwa sababu kilipata hati ya kumiliki ardhi miaka 10 kabla ya kuanzishwa.

“Jaji Werema alishauri kuwa kijiji hicho kilipewa hati Na. MG/KJJ.522 ya Juni 16, 1999, hivyo kutaka aliyeghushi achukuliwe.”

Hamis amefafanua kuwa barua hiyo, ilikuja siku chache kabla ya maafa ya kuchomwa nyumba 40 na vifo vya wakulima wawili na mfugaji mmoja.

Ushauri wa Jaji Werema ulitokana na barua ya Waziri Mkuu Kumb. PM/P/1/569/29 ya Mei 8, 2014 kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na kunakiliwa kwa AG.

Taarifa zilizopo ni kwamba Jaji Werema na Bendera walikutana mara mbili kujadili mgogoro huo kabla ya kutoa ushauri huo wa kutaka hatua zichukuliwe haraka.
Katika uchambuzi wa kesi za hukumu za Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa kuhusu mgogoro wa ardhi kati ya kijiji cha Mabwegere na vijiji jirani, Jaji Werema alitaja mambo muhimu aliyogundua juu ya hukumu hizo.

Anasema “Mahakama haikutoa uamuzi wowote kuhusu uhalali wa kuanzishwa kwa kijiji cha Mabwegere, Mahakama haikuilekeza halmashauri ya wilaya ya Kilosa kuipa hadhi ya ‘kijiji’ Mabwegere, jukumu alisema sio la mahakama.

Mahakama iliamua kwamba, hati ya kumiliki ardhi iliyotolewa kwa kijiji cha Mabwegere ni hati halali na mahakama iliamuru kwamba, haukutolewa ushahidi wa kuthibitisha kwamba, Hamis Msabaha na wenzake 37, walivamia kijiji cha Mabwegere.”

error: Content is protected !!