Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yazindua Sera mbadala ya maendeleo ya Taifa
Habari za Siasa

Chadema yazindua Sera mbadala ya maendeleo ya Taifa

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua sera mbadala ya Taifa leo Jumanne tarehe 25 Septemba, 2018.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe amesema hii ni mara ya pili kwa chama chake kuandaa na kuzindua sera mbadala ya taifa tangu kuanzishwa kwa chama hicho mwaka 1992.

“Mwanzoni mwa mwaka 1990 waasisi wa chama hiki, mimi nikiwa ni mmoja wao na ndio nilikuwa mdogo kuliko wote, tuliona siasa za ujamaa ambazo ndiyo ilikuwa sera ya CCM, hazifai na haziwezi kuwapelekea maendeleo Watanzania. Kwa pamoja tukaamua njia pekee ni kuanzisha vuguvugu la vyama vingi tukiamini kama serikali itakubali, basi tuanzishe chama cha siasa ambacho kitakuwa na sera mbadala ya ile ya ujamaa.

“Kwa hiyo mfumo wa vyama vingi ulikubaliwa, haraka tulisajili chama cha siasa cha CHADEMA na ilipofika mwaka 1993, mara tu ya kupata cheti cha usajili, tuliandaa Sera mbadala ya taifa ya mlengo wa kati ambayo ilikuwa inatofautia na ile ya ujamaa,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo ambaye ni Mbunge wa jimbo la Hai, amesema baada ya kuiandaa sera ya chama chao, walimpelekea Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ambaye baada ya kuisoma aliikubali na kusema kuwa sera hiyo ndiyo hasa italeta maendeleo kwa Watanzania.

Akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati kuu ya Chadema wakiwemo Mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, Wabunge wanaotokana na chama hicho, wageni waalikwa wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali na wananchi wa kawaida, Mbowe alisema baada ya miaka 25, chama chake kimeamua kuandaa tena sera mbadala ya taifa.

“Chama changu kimeamua kuandaa tena Sera hizi ambazo tumegusia Nyanja 12 ambazo tuna Imani zina tija kwa maslahi mapana ya wananchi na taifa kwa ujumla wake.

“Tumegusia Katiba, Utawala, Uchumi wa Soko Jamii, Siasa za ndani, Siasa za Kijamii na Afya. Lakini pia tumeangazia kwenye masuala ya Usimamizi wa ardhi, Kilimo, Miundombinu, Mazingira na mambo ya nje. Na hii sera yetu tunaiweka wazi kwa umma ili Watanzania wajue nini tunachokipigania kwenye hii nchi,” aliongeza Mbowe.

Baada ya kuzindua Sera hiyo, Mbowe amesema chama chake kimefungua rasmi milango ya kupokea maoni na ushauri juu ya sera hiyo kutoka kwenye vyama vya siasa, mashirika ya umma, taasisi mbalimbali na raia wa kawaida.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!