Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yazindua ‘Join the Chain,’ Lissu aeleza malengo
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yazindua ‘Join the Chain,’ Lissu aeleza malengo

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

CHAMA kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, kimezindua program maalum iitwayo ‘Join the Chain’ yenye lengo la kukusanya fedha za ujenzi wa demokrasia kutoka kwa kila mmoja wa ndani na nje ya nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Uzinduzi huo umefanywa kupitia mtandao ‘Zoom’ leo Ijumaa, tarehe 25 Februari 2022 na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho-Bara, Tundu Lissu na kufuatiliwa na watu mbalimbali kupitia Youtube, Twitter, ClubHouse na mitandao mingine.

“Tunazindua Join the Chain, itakayomwezesha kila mmoja kushiriki kujenga demokrasia imara katika nchi yetu. Kila mmoja wetu ina maana kila Mtanzania bila kujali itikadi ya kisiasa, dini, umri, kabila, rangi, yupo ndani au nje ya Tanzania atashiriki,” amesema Lissu aliyeko Ubelgiji

Lissu amesema, “kila mmoja wet na yoyote yule mwenye uhusiano wa aina yoyote ile na nchi yetu ya Tanzania, mwenye nia njema kwa nchi na chama chetu. Tunaposema Join the Chain, tunataka kuunganisha nguvu za kila mmoja ili tujenge demokrasia imara.”

“Bila demokrasia hatuko salama, awe raia wa Tanzania au asiywe raia wa Tanzania bila demokrasia hakuna mtu aliye salama na ndiyo maana na ndiyo maana tumeanzisha Join the Chain ili kuunganisha nguvu ya kila mmoja,” amesema.

Amesema, ili kujenga demokrasia imara, kila mmoja ajiunge Join the Chain, atoe mchango wake kwani wapo watakaosimama majukwaani wanahitaji wawekewe vyombo ili waongee, wapo watakaofanya kazi mitaani na mashambani walipo wananchi wanahitaji kuwezeshwa, wapo watakaohitaji kututetea mahakamani, watahitaji kuwezeshwa, wapo watakaoumia watahitaji kutibiwa, wapo watakaotozwa faini kubwa watahitaji kusaidiwa kulipa fidia.

“Kama unaweza kutoa Sh.1,000 au Sh500 ya zaka au sadaka kanisani au msikitini, tunakuomba utoe chochote katika hii kazi ya kujenga demokrasia imara ili kila mmoja awe na amani katika biashara, makazi na nchi yetu,” amesema

“Sisi Chadema tuko zaidi ya milioni saba, kila mmoja tu akichanga Sh.1,000 tutakuwa na fedha kiasi gani ya kuwezesha kununua bendera, vyombo vya usafiri, maji na chakula ili watu wafanye kazi ya ujenzi wa demokrasia nchi nzima inawezekana,” amesema Lissu

Aidha, Lissu amesema chama hicho hakichukui fedha za ruzuku zinazotokana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hivyo ili kuendelea na ujenzi wa demokrasia inahitajika fedha kwani rasilimali watu wapo wa kutosha.

Ametumia fursa hiyo kusisitiza kwamba yeye pamoja na wajumbe wa kamati kuu, Godbless Leman a Ezekiel Wenje waliopo uhamishoni “tuliokimbia nchi kwa sababu mbalimbali tunarudi nyumbani. Nitakuja nyumbani, mimi Lema, Wenje na wengine tutakuja nyumbani kujenga demokrasia imara.”

Awali, mwenyekiti wa kamati ndogo ya Join the Chain, Godbless Lema aliyeko nchini Canada alisema “kwa sasa Chadema haiko Ikungi, Dodoma ama Arusha pekee, kinakubalika maeneo mbalimbali dunia.”

“Chadema ina watu zaidi ya mara mbili ya wana CCM na katika kuliona hilo tukabaini Chadema haina shida ya watu bali ni fedha. Ili watu waweze kutembea maeneo mbalimbali nchini ndiyo tukaja na hii Join the Chain, tunataka kila mmoja aone wajibu wa kuchangia kidogo inaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye nchi yetu,” amesema

Mbunge huyo wa zamani wa Arusha Mjini, amesema “tunataka kuanza kutengeneza mnyororo huu, mfano mtu ukiacha kunywa bia moja tu na kuchangia kidogo, tunaweza kuwa na fedha nyingi, kwani tuna Baraza Kuu mwezi wa nne na operesheni itakayofanyika nchi nzima baada ya makamu mwenyekiti (Tundu Lissu) atakaporejea nchini.”

Lema amesema, “tunazindua programu maalum ya kuwaunganisha wananchi na wana Chadema pande zote za dunia kwani Chadema ni imani na ni matumaini. Tunaamini katika nguvu ya umma na katika mapito tunayopitia tutavuka tukiwa pamoja kupitia Join the Chain kwani Shilingi yetu ndiyo nguvu yetu.”

4 Comments

  • Excellent move. Tumekwama kama nchi. Tunahitaji kujinasua na njia pekee ni kuboresha governance na democracy.

  • Grazie ndugu lissu lakini hujajitambua kama umma umeshakutambua ndugu lissu kuwa hauna uwezo wa kujiongoza wala kuongoza

  • Hakuna chama kikngine cha siasa kinachoweza kuunganisha na kuweka pamoja demokrasia na maendeleo, isipokuwa CHADEMA. Maendeleo bila demokrasia ni maendeleo yasiyotokana na mamlaka ya wananchi bali yanalazimishwa kwa wananchi bila ridhaa yao; demokrasia bila maendeleo ni kejeli inayopumbaza watu wasifikirie ustawi wao!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!