March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yazidi kumtekenya Magufuli, wasema anahusika kumdhuru Lissu

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeituhumu serikali ya rais John Magufuli kuwa inahusika na tukio la shambulio la kifo dhidi ya Tundu Lissu, anaandika Hellen Sisya.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo katika mtaa wa Ufipa Kinondoni jijini Dar es salaam, Benson Kigaila, Mkurugenzi wa Mafunzo wa chama hicho amesema kuwa kuna baadhi ya matukio ambayo yanathibitisha kuwa serikali inahusika.

Amesema kauli ya Rais Magufuli aliyoitoa mwaka jana akiwa katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani wa Singida kwamba ifikapo mwaka 2020 hakutakuwa na upinzani nchini.

“Lakini hakuishia hapo.baada ya pale yakaanza matamko ya kuzuia shughuli za vyama vya kisiasa jambo ambalo ni kinyume cha sheria zilizopo, lakini cha pili, wakaanza kukamatwa watu mbalimbali, yeyote anayeikosoa serikali ya Magufuli, ameishia kwenye mikono ya dola. na Lissu amekuwa mahabusu, amekuwa mahakamani kila uchwao,” aliongeza Kigaila.

error: Content is protected !!