January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yaweka wazi msimamo kuhusu midahalo

Spread the love

CHAMA cha Demokrasi na Maelendeleo (Chadema), kimetoa ufafanuzi wa suala la kutohudhuria kwa mgombea urais kupitia mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa katika Mdahalo wa Mgombea urais uliondaliwa na Taasisi ya Twaweza pamoja na Tanzania Media Foundition. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Hayo yameelezwa na Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene alipokua akijibu maswali ya waandishi wa habari katika ufunguzi wa kituo kipya cha mikutano ya waandishi wa habari cha UKAWA,amesema kuwa mdahalo huo haukidhi viwango vya ubora wa kuweza kuwapima vizuri wagombea

Akitaja vigezo vya midahalo mikubwa ya mgombea urais amesema kuwa kigezo hawakuweka kigezo cha wagombea kuulizana maswali,pia waandaaji hao hawana sifa ya kuandaa midahalo kutokana kukosewa imani na umoja huo kwa kutoa tathimin zinazobeba upande mmoja ambao ni wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM).

Aidha Makene aliwashangaa waandaji wa midahalo ambao tayari wameshajipambanua kuwaunga mkono wagombea wengine halafu wanajificha katika pazia kuandaa midahalo ili kuhadaa umma wa watanzania.

Hivi karibuni, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilimkataza mgombea wake Edward Lowassa kuhuduria mkutano ulioandaliwa na Taasisi Watendaji wakuu wa makampuni (CEORT) baada ya Mwenyekiti wake Ali Mfuruki kujipambanua kumuunga mkono John Magufuli mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi.

Mmoja ya waandaaji wa mdahalo wa marais, akiwa katika kampeni ya mmoja wa mgombea Urais
Mmoja ya waandaaji wa mdahalo wa marais, akiwa katika kampeni ya mmoja wa mgombea Urais

“Nchi ya marekani na nchi nyengine wanakuwa na Taasisi maalum zenye kuamika ambazo huanda midahalo iliyo bora na yenye vigezo bila kukibeba chama fulani” amesema Makene.

Wiki hii katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere kulifanyika mdahalo uliorushwa na kituo cha televisheni cha Star tv uliohudhuliwa na wagombea wanne ambao ni Chief Lutaselo Yemba wa chama cha Allience For Democry Change (ADC), Anna Mghwira wa ACT-Wazalendo, Maximilan Lyimo wa Tanzania Labour Party (TLP) na Mgombea aliyechelewa kufika kutokana na alichodai ni kuchelewa njia, Hashim Rungwe wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

error: Content is protected !!