Saturday , 2 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yawatibua ‘Kigogo’, Sarungi, Zitto 
Habari za Siasa

Chadema yawatibua ‘Kigogo’, Sarungi, Zitto 

Spread the love

HATUA ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kuomba Rais wa Jamhuri, Dk. John Pombe Magufuli, kile alichoita, “maridhiano ya kitaifa,” imewatibua baadhi ya wanasiasa wenzake na wanaharakati. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). 

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika, jana jijini Mwanza, Mbowe alimtaka Rais Magufuli, kutengeneza maridhiano ya kitaifa, ili kuweza kulikwamua taifa.

Alisema, “nimekuja kushiriki, kama uthibitisho wa ulazima kuwepo maridhiano, upendo na mshikamano kwa taifa letu. Tuvumiliane, tukosoane na turuhusu demokrasia; rais una nafasi ya kipekee kujenga maridhiano katika taifa.” 

Kauli hiyo, kwa kuzingatia mazingira hasi ya siasa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji wa mwaka 2019, Vijibaadhi ya wanaharakati wamedai Mbowe ameonesha kuelemewa.

Akiandika katika ukurasa wake wa twitter, Fatma Karume, mmoja wa wanasheria mashuhuri nchini na mtoto wa aliyekuwa rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, amehoji na kusema, “Hebu tuache kulumbana.”

Ameongeza: “Nina swali moja tu kwa CDM (Chadema). Kwamba, baada ya kupewa dakika moja ya kusema leo, na mkatoa maombi yenu, Magufuli (Rais Magufuli) alijibu vipi?”

Naye mwanaharakati mashuhuri anayejitambulisha kwa jina la Kigogo2014@, ameonesha kuchukizwa kwake na hatua ya Mbowe kuomba maridhiano.

Anasema, “wanaomba kwa kuwa wamebanwa wamelegea, hawaobi mbele na maarifa yamewaishia! Lazima sasa waombe huku wamefyata mkia.”

Amesema, “kwangu maridhiano ni kurudi na kulinda misingi ya haya yakiyoandikwa kwenye Katiba ya JMT (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Kwa upande wake, Zitto Zuberi Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, ameandika katika ukurasa wake wa twitter, kwamba upinzani uliomba maridhiani kabla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na haikuwa hivyo.

Anasema, “…tulitaka maridhiano ya kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa ili kuwe na uchaguzi huru. Tukawaondoa wanachama wetu vijijini.

“Leo mnataka mkae mezani na CCM (Chama Cha Mapinduzi), ili kuokoa viti vyenu bungeni, halafu muwaache solemba malaki ya wanachama waliojitoa vijijini?”

Mwanaharakati mwingine Maria Sarungi, kwenye ukurasa wa twitter, amekumbushia namna mwanaharakati wa Marekani, alivyoendesha mapambano bila ‘kuchutama.’

“Martin Luther King Jr alishinda tuzo ya Nobel, ila tokea mwaka 1955 hadi alipouwawa mwaka 1968, King alikuwa anaendelea kuandamana, kukamatwa, kufungwa. Alielewa kupata uhuru wa kweli na haki si kuacha misingi.”

Hata hivyo, mtu anayejitambulisha kwa jina la @Seneta_Kibanga ametetea uamuzi wa Mbowe na chama chake na kusema:

“Fatma, Nakuheshimu sana, lakini sisi mashabiki kutafuta makosa kwenye uamuzi wa CDM (Chadema) wa kushiriki sherehe za Uhuru, ni unafiki. Mbowe ameshakaa rumande miezi mingapi? Tulimsaidiaje? Lema? Sugu? Au tulitweet tu na hakuna lilitokea? Tuwaache Chadema wawe huru kubadilia mbinu zao.”

Erick Nyagawa, akimjibu Karume amesema: “Awe amejibu hajajibu, ujumbe umefika…Watanzania wanalilia demokrasia ya kweli.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia kuzindua programu ya nishati safi ya kupikia kwa wanawake Afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua programu ya...

Habari za Siasa

AG aiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia mawakili wanaokiuka maadili

Spread the loveMWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Dk. Eliezer Feleshi, ameagiza Kamati...

Habari za Siasa

Jaji avunja ukimya sakata la Mpoki kusimamishwa uwakili

Spread the loveJAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amekitaka Chama cha...

Habari za Siasa

Sheikh Ponda ataka mwarobaini changamoto uchaguzi 2020

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa...

error: Content is protected !!