July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yawaonya wanaowachafua wenzao

Kada wa Chadema, Philipo Mwakibinga

Spread the love

KADA wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Philipo Mwakibinga amewakemea baadhi ya watu ambao wanatumia siasa za maji taka kutoa taarifa za uzushi na za kuchafuana. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mwakibinga ambaye ni Afisa Mafunzo Chadema Taifa na mtangaza nia ya ubunge katika jimbo la Lipa mkoani Mbeya amesema vitendo vya baadhi ya wanasiasa kutoa taarifa za uzushi juu ya wapinzani wao ni dalili za kukosa sera.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amesema amesikitishwa na baadhi ya watu ambao wanatumia muda wao mwingi kutunga habari za uzushi kwa wana siasa hususani wa Chadema kuwa wamehama chama na kujiunga ACT.

Mwakibinga amesema kuwa wapo watu ambao wanakosa sera za za kisiasa na kuamua kuwachafua watu wengine kwa kuwapakazia mambo ambayo hayana kichwa wala miguu.

Akizungumzia suala la yeye kupakaziwa kuwa ameamia ACT Wazalendo amesema jambo hilo siyo kweli na kamwe hawezi kufanya ujinga huo.

“Mimi ni mwanachana wa Chadema na nitahakikisha nakitumikia chama kwa nguvu zangu zote na akili zangu zote sina mpango wa kukihama chama na ikumbukwe kuwa mimi nimetia nia ya kugombea jimbo la Chunya na nimeshika nafasi ya tatu.

“Ninajua kila mtyu anajua uwezo wangu wa kimapambano katika chama lakini kama haitoshi Chadema inakuwa usiku na mchana leo hii niondoke chadema niende wapi ambapo kuna demokrasia kubwa kama chadema”? alihoji Mwakibinga.

Mbali hilo Mwakibinga aliwataka watanzania ambao ni wapenda mageuzi kuhakikisha wanakuwa watulivu katika mchakato wa kutangaza rais ambaye atapeoperusha bendera ya ukawa.

Amesema kujiunga kwa Waziri Mstaafu Edward Lowasa Chadema ni dalili nzuri ambazo zinaonesha kuwa CCM imechoka na inaelekea kuondolewa madarakani kwa njia ya kidemokrasia bila kumwaga damu.

Amesema kutokana na hofu ya viongozi wa CCM wameanza kutengeneza mikakati ya kutaka kuwadhoofisha watanzania wapenda maendeleo kwa kutunga uongo kwa madai kuwa kwa sasa wapo viongozi makini ndani ya Chadema ambao wanaondoka katika chama na kujiunga na vyama vingine vya siasa.

“Ndugu zangu watanzania naomba msisikilize maneno ya wazushi ambao wameishiwa sera hakuna kiongozi makini ambaye anaweza kuondoka Chadema tunapambana na adui ambaye ni CCM na ni lazima tumshinde kwa tena kwa kishindo kikubwa” amesema Mwakibinga.

error: Content is protected !!