December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yawaita Watanzania kumpokea Lissu

Benson Kigaila, Naibu Katibu Mkuu Chadema Bara

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nchini Tanzania, kimewakaribisha wanachama, vongozi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kumpokea Tundu Lissu, makamu mwenyekiti wa chama hicho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam…(endelea).

Lissu anarejea nchini Tanzania Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 saa 7:30 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere akitokea Ubelgiji.

Lissu amekuwa nje ya Tanzania tangu tarehe 7 Septemba, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa nje ya makazi yake Area D jijini Dodoma.

Alifikwa na mkasa huo mchana wakati akitoka kuhudhuria mkutano wa Bunge uliokuwa ukiendelea.

         Soma zaidi:-

Baada ya kushambuliwa, Lissu alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kwa matibabu ya awali na usiku huo huo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Lissu alipata matibabu hospitalini hapo hadi tarehe 6 Januari 2018 alipohamishiwa nchini Ubelgiji kwa matibabu na tayari amekwisha kueleza yeye mwenyewe amepona.

Leo Jumamosi tarehe 25 Julai 2020, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, Benson Kigaila amesema, kupona kwa Lissu ni muujiza hivyo, kila mmoja mwenye nafasi ajitokeze kumpokea.

“Tunawaalika Watanzania, wanachama wa Chadema, viongozi na Watanzania kuja kumpokea Lissu ambaye atarejea anatembea kwa miguu mwili, kuliko kipindi anaondoka hatukujua kama atarudi au atakuwa na saa mbili zaidi za kuwa hai,”

“Tunawakaribisha na kuwaomba wajitokeze kumpokea. Kwenda kumpokea ni kutoa shukrani kwa Mungu kwa kumfanya kuendelea kuwa hai anaporejea kuungana nasi katika mapambano ya kudai demokrasia,” amesema Kigaila.

error: Content is protected !!