May 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Chadema ‘yavuna’ kutoka NCCR-Mageuzi

Spread the love

FELIX Mkosamali, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, ametangaza kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka mkoani humo zimeeleza, Mkosamali ametangaza kuhama NCCR-Mageuzi leo tarehe 18 Juni 2020 jijini Dar es Salaam, na kuongeza anatarajia kugombea jimbo hilo kupitia chama hicho.

“Ninajiunga na Chadema na nina mpango wa kugombea ubunge kupitia chama hicho,” amesema Mkosamali wakati akitangaza kujiunga na Chadema.

Mwaka 2017, Mosamali alikituhumu chama chake cha awali kwamba kimepoteza dira, na kuwa kimemezwa na Chadema.

Pia amekituhumu chama NCCR-Mageuzi kwamba kimepoteza dira baada ya kukumbatia waliokuwa mafisadi wanaohamia kwenye vyama hivyo kutoka CCM.

“Nimehama chama cha NCCR-Mageuzi kwasababu kimekuwa kama kinyonga hakieleweki kipo CCM au upinzani, ni chama ambacho kimekuwa hakifanyi kazi yoyote ya kisiasa kwa miaka mitano sasa kimeanza kuweka wagombea kwenye majimbo ya Chadema,” amesema na kuongeza.

“Nimeona Chadema ndio chama sahihi kugombea ubunge kwasababu kuna wanasiasa wenye msiamamo wa kiasaiasa na wenye kudai katiba mpya”.

Amesema kuwa amekihama chama hicho ili aendelee kupigania mambo ya msingi na si kujipendekeza na kuwa anaamini wanaohama vyama ni haki yao lakini wengi wanaitumia vibaya haki hiyo kwasababu ya njaa na kushibisha matumbo yao.

“Wengi wanaohama Chadema kiu yao ni kuongoza lakini kama mtu unapigania mageuzi aeleze hoja sio kuunga juhudi kwasababu reli au ndege zimenunuliwa, ukisikiliza ni hoja dhaifu wanahama kwa kutafuta madaraka na pesa mimi sinunuliwi”.

error: Content is protected !!