July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Chadema yatwaa Mji mdogo Katoro

Mwenyekiti wa CDM Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr. Wilbrod Slaa wakiteta

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimechaguliwa kuuongoza Mji Mdogo wa Katoro mkoani Geita, baada ya kukibwaga Chama Cha Mapinduzi (CCM). Anaandika Mwandishi wetu…(endelea).

Mkurugenzi wa Halmashauli ya Wilaya ya Geita, Ali Kidwaka amesema kuwa Chadema imepata kura 38 dhidi ya 29 za CCM kati ya kura zote 67.

Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti walikuwa ni Zakaria Lulengo (CCM) na Japhet Mdoshi (Chadema). Kwa mujibu wa Kidwaka, nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Isack Charles wa Chadema naye alipata kura 38 na hivyo kumbwaga Emanuel Daudi wa CCM aliyeambulia kura 29.

Kamati mbalimbali zimeundwa, ambazo ni Fedha Utawala na Mipango Miji, Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Elimu, Afya na Maji na kamati ya Ukimwi.

error: Content is protected !!