Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yatoa ratiba wagombea urais, ubunge na udiwani
Habari za Siasa

Chadema yatoa ratiba wagombea urais, ubunge na udiwani

Reginald Munisi, Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimefungua zoezi la uchukuaji fomu za kugombea Urais wa Tanzania, ubunge na udiwani, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ratiba hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 29 Juni 2020 na Reginald Munisi, Mkurugenzi wa Uchaguzi Chadema, wakati anazungumza na waandishi wa habari, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Munisi amesema, zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu ya urais wa Tanzania, litafanyika kuanzia tarehe 4 hadi 19 Julai 2020.

Amesema wenye nia ya kugombea nafasi hiyo, wanapaswa kufika katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, kwa ajili ya kuchukua fomu, kisha kutafuta wadhamini 100 kwa kila kanda kumi za chama hicho.

“Mchakato wa mgombea urais utakuwa wazi kuchukua fomu kuanzia tarehe 4 Julai mwaka huu, wenye nia ya kugombea ama wao au mawakala wao watafika makao makuu. Na kuchukua fomu kutoka ofisi ya katibu mkuu, “ amesema Munisi.

“Siku ya tarehe 19 Julai saa 10:00 jioni wagombea wawe wamekamilisha ujazaji fomu na udhamini walete kwa katibu mkuu.”

Munisi amesema, wagombea wanatakiwa kutafuta wadhamini katika kanda zote za Chadema, ambazo ziko 10. Kwa sharti la wadhamini kutokuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.

“Baada ya kuchukua fomu, watakua na muda wa kujaza na kuomba mdhamini, mgombea uraisi au wakala wake, baada ya kuchukua fomu, ataenda kutafuta wadhamini kwenye kanda zetu zote kumi. Kila mgombea kwenye kila kanda apate wadhamini wasiopungua 100,” amesema Munisi.

    Soma zaidi:-

Munisi amesema, “sharti si mwanachama tu ndiye anayefaa kuwa mdhamini, lakini mwanachama asiwe mjumbe wa  mkutano mkuu wa chama, ambao mwisho wa siku atapiga kura ni nani awe mpeperusha bendera wetu wa uchaguzi wa urais. Wajumbe wa mkutano mkuu wasubiri muda wao kwenye.”

Baada ya zoezi la uchukuaji na ujazaji fomu kukamilika, tarehe 22 Julai 2020 Katibu Mkuu wa Chadema atawasilisha taarifa za watia nia katika mkutano wa kamati kuu ili lipendekeze wanaofaa kuingia katika hatua inayofuata.

“Kamati Kuu itafanya maamuzi, kuchakata taarifa na kupendekeza majina ya waliojaza fomu, kwenda baraza kuu ili liseme nani anafaa , kamati kuu ikimaliza inapeleka baraza kuu jina moja au zaidi, baraza kuu linachakata, linaamua nani aende hatua zinazofuta, ambapo ni kikao cha uteuzi ambapo ni mkutano mkuu,” amesema Munisi.

Munisi amesema, baada ya Baraza Kuu la Chadema kupendekeza majina hayo, itayapeleka kwenye Mkutano Mkuu wa chama hicho, unatarajiwa kufanyika tarehe 29 Julai 2020. Ambao utapitisha jina la mgombea urais wa Chadema.

“Mkutano mkuu wetu unatarajia kufanyika mwisho mwa mwezi Julai, mkutano mkuu utakaa tarehe  29 Julai 2020, utaamua nani atapeperusha  bendera kwa niaba ya Chadema,” amesema Munisi.

Zoezi hilo litawahusu wanachama wote wenye sifa pasina kujali kama alitia nia au hakutia nia ya kugombea urais ndani ya chama hicho kikuu cha upianzani nchini.

Waliokwisha tia nia ya kuwania nafasi hiyo ni;

  1. Isaya Mwita
  2. Lissu Tundu A.M
  3. Dk. Majinge, Mayrose Kavura
  4. Manyama Leonard Toja
  5. Mbowe, Freeman Aikael
  6. Mchungaji Msigwa, Peter Simon
  7. Wakili.  Mwanalyela, Gasper Nicodemus
  8. Nalo, Opiyo G.O.M
  9. Wakili Neo, Simba Richmund
  10. Shaban, Msafiri
  11. Lazaro Nyalandu

Kuhusu mchakato wa utafutaji wagombea ubunge, Munisi amesema zoezi hilo litaanza rasmi tarehe 4 hadi 10 Julai 2020 kwa wanaotaka kugombea kuchukua fomu ofisi za majimbo, kanda au mitandoni kisha kuzijaza na kuzirejesha ofisi ya jimbo analogombea.

Munisi amesema, udiwani, uchukuaji na urejeshaji fomu utaanza Julai 11 hadi 17 Julai 2020. Fomu zitapatikana ofisi za kata na mitandoni.

Kuhusu viti maalum uchukuaji na urejeshaji wa fomu zitaanza kutolewa Julai  4 hadi 19, 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!