Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CHADEMA yatikiswa, wengine mbioni kung’oka
Habari za SiasaTangulizi

CHADEMA yatikiswa, wengine mbioni kung’oka

Wanachama wapya wa CCM waliojiunga na chama hicho wakitokea upinzani
Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kinaweza kukimbiwa na viongozi wake wengine watatu, wakiwamo wabunge wawili wa majimbo, anaandika Mwandishi Wetu.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho na Ikulu jijini Dar es Salaam zinasema, mkakati mkali unasukwa wa kuwashawishi viongozi hao kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hata hivyo, mmoja wa viongozi anayeshawishiwa kuondoka amenukuliwa akisema, hajafikiria kufanya hivyo na kwamba hata ikimbidi kuondoka ndani ya Chadema, hatajiunga na CCM, bali atafanya shughuli zake binafsi.

Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja muda mchache baaada ya mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Pastrobas Katambi kujiunga na CCM leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Aidha, kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja wiki tatu baada ya gazeti hili kuripoti kuwapo kwa mpango wa wabunge wa viongozi wa Chadema kukima chama hicho.

SOMA: Upinzani kupata pigo

1 Comment

  • Hakuna kitu apo, hata angehama Mbowe bado CDM Haitakufa watu wenye akili timamu ndi wanakuja kama Mhe Nyalandu, hatuangalii mtu na utashi wake kama patrobas ameshindwa kuitumikia nafasi yake njia iko wazi watakuja wengine.Hata kwenye kanisa watu wanaokoka na kurudi nyuma sembuse siasaAMERUDI KWENYE MATAPUTAPU HUYU, AMERUDIA MATAPISHI YAKE MWENYEWE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

error: Content is protected !!